Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillus Wambura amewataka
askari Polisi kuelendea kufanya kazi kwa
kuzingatia tunu za Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na nidhamu, haki, weledi na uadilifu.
IGP Wambura ameyasema hayo Mei 18, 2024 wakati akiwavisha
Nishani Maafisa, Wakaguzi na Askari Polisi 27 wa vyeo mbalimbali Jijini Dar es
Salaam.
Aidha, IGP Wambura
amesema dhamira ya Jeshi la Polisi ni kuwa na Jeshi bora la kisasa na la
mfano wa kuigwa lenye kutoa huduma sahihi na stahili kwa wananchi.
Katika hatua nyingine amewataka askari kutambua namna ambayo
serikali imeamua kuboresha Jeshi hilo na hivyo kufanya kazi kwa bidii, weledi,
nidhamu, uaminifu na uadilifu.
"Tujiweke katika kutoa huduma zinazolenga kupunguza
malalamiko. Pia askari kutenda kama wenye mali katika kutekeleza majukumu ya
kila siku" Alisema.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi ya
Dar es Salaam, SACP Muliro J. Muliro, kwa niaba ya maafisa, wakaguzi na Askari
waliovishwa nishani leo amesema Nishani
hizo ni chachu ya kujenga morali kwa askari kuendelea kutekeleza majukumu yao
kwa weledi na usahihi.
Aidha amesema
"tunashukuru sana kwa nishani hizi kwani
Amir Jeshi Mkuu na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura wameona na kutambua mchango wetu" alisema.
SACP Muliro aliongeza kuwa "Sisi tunaahidi kutenda kwa
weledi na kuzingatia sheria, haki na kuwatumikia wananchi kwa kuwafanya
wanakuwa salama"
IGP Wambura amewavisha nishani askari 27 kwa niaba ya Askari 1247 wa Kanda ya Mashariki ikihusisha Mkoa wa Pwani, Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Mkoa wa Rufiji walitunukiwa nishani hizo na Amir Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
.jpeg)




Post a Comment