Na.Timothy Marko
HALIMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imeweza kusanya Shilingi bilioni 95 kwakipindi kinachoishia Mwezi Juni huku jiji hilo lina lenga kusanya bilioni 20 Mwishoni mwezi Juni Mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mchumi wa Halimashauri hiyo Julias Mdeme amesema kuwa Halimashauri hiyo imelenga kufanya maboresho ya Usafiri wa Mwendokasi (BRT).
"Tumelenga kujenga Shule za Msingi na Sekondari za Ghorofa katika maeneo ya Tabata Kimanga,na Vingunguti"Alisema Julis Mdeme
Mchumi Julias Mdeme ameongeza kuwa pia Halimashauri hiyo imetenga Shilingi bilioni 40 kwa ajili ya Masoko ilikuchochea Biashara.
"Tunataka Dar es Salaam iakisi Mazingira Salama ,lakini BRT bado si Salama"Aliongeza Mchumi wa Mkoa Dar es Salaam Julias Mdeme.

Post a Comment