LHRC YAWAPIGA MSASA WANAHABARI

***************
Na Mwandishi Wetu -Dodoma

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu  (LHRC), kimewapa semina ya siku mbili kwa waandishi mbalimbali wa habari hapa nchini yenye lengo la kuwajengea uelewa juu ya taarifa zinazohusu mauaji ya wenza.

Semina hiyo  imeanza leo jijini Dodoma, huku pia ikilenga kuwapa elimu hiyo ambayo itakuwa chanya katika kuandika habari  zinazohusu mauaji ya wenza ,ukatili wa kijinsia,Viashiria hatarishi vya ukatili.

Kwa siku ya kwanza Mafunzo hayo yatahusu madhara ya mauaji ya wenza , maana ya mauaji ya wenza kwa Tanzania,Taarifa ya ripoti maalumu ya mauaji ya wenza ,Taarifa ya Haki za Binadaamu kuhusu mauaji ya wenza jinsi athari zake zinavyoathiri makundi mbalimbali.

Katika  hatua nyingine kwa siku ya pili mafunzo hayo yatahusu Sheria kuhusu ukatili  na mauaji ya wenza,utoaji habari zenye kuzingatia hali ya wahanga na mifano ya habari mbalimbali nzuri na mbaya lugha nzuri ya kutumia masuala ya jinsia.












                                         
                   (PICHA ZOTE NA JOHN SIMWANZA)

0/Post a Comment/Comments