
*******
Na.Timothy Marko
MAENDELEO Benki imetoa mikopo ya Shilingi
Bilioni 9.8 katika kuwawezesha Wafanyabiashara wadogowadogo wapatao700 wa jiji
la Dar es salaam itakayo wawezesha kupata Maakaazi ya Nyumba
500.
Akizungumza waandishi wa Habar jijini Dar es
Salaam Mkurugenzi wa Maendeleo Benki Ibrahim Mwangalaba, amesema mpango huo utawezesha
wamachinga kumiliki ardhi na Makazi bora
ili kuliwezesha kundi hilo kukopesheka kwenye Mabenki.
" Kwa mpango huu utawawezesha kukidhi
vigezo vya kukopesheka ili kukuza mitaji
kwa sababu watakuwa wanakidhi Sharti la Uwepo wa dhamana ya mikopo
ambayo ndio limekuwa kikwazo kikubwa cha kukopesheka kwa wamachinga walio
wengi"Alisema Mkurugenzi Ibrahimu Mwangalaba.
Mwangalaba aliongeza kuwaDhamira ya Benki hiyo
nikuwainua Wamachinga na wafanyabiashara wadogowawogo kutoka kwenye nafasi hiyo
kwenda kuwa wafanyabishara wakubwa.
Alisisitza kuwa Hatua hiyo itawezesha ukuaji
wa Uchumi na Uzaliishaji na ulipaji wakodi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wamachinga wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Namoto Yussufu Namoto, amesema kuwa wafanyabiashara hao
wametengeneza kanzi data ya wafanyabiashara wa mkoa huo ambapo zaidi masoko17
yanatambulika najumuya hiyo.
Alisema Hadi kufika Mwezi huu zaidi ya
shilingi bilionj19.2 zimeweza kukopeshwa kwa wafanyabishara hao.
"Wamachinga 700 wamekopeshwa viwanja
milioni 500 vyenye thamani ya shilingi bilioni 10"Alisema Mwenyekiti wa
wamachinga mkoa wa Dar es salaam Namoto
yusufu





Post a Comment