*******
.
Timothy Marko
MBUNGE wa Jimbo la Kisesa Luhaga Mpina Ameuomba Umoja wa Afrika (AU) Kuridhia Uanzishwaji wa Tume Maalum itakayoshughulikia Matatizo sugu ya Bara hilo ili kuleta Utengamano wa kisiasa.
Akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje Bungeni Dodoma Luhaga Mpina amesema kuwa licha ya kuwepo jumuhia zakikanda mbali zinazo jihusisha Ulinzi wa Amani ikiwemo Au, EAC,SADC,naNyinginezo kumekuwa Mapigano Makali Ambayo yamesasababisha Mapinduzi katika Nchi za Burkinafaso,Mali ,Gabon Niger, Sudan Nchi hizo hazikupaswa kusimamishwa na badala yake Jumuhia hiyo ingezishauri Nchi hizo kuzingatia Utawala wa Sheria.
"Licha ya Utajiri wa Gesi,Mafuta, Bandari lakini Bara la Afrika limekuwa likabililiwa na kukosekana Sera na Sheria Madhubuti za kulinda Ajira"Alisema Mbunge Huyo Luhaga Mpina.
Mpina aliongeza kuwa sambamba na ukosefu wa Sera Madhubuti wa nchi hizo pia Bara Afrika limekuwa likabiliwa na Matatizo ya Magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo Figo ,Moyo na kisukari.
Alisitiza kuwa ni Vyema bara la Afrika likatafuta mwarobaini wa Matatatizo ya bara hilo.
"Nimuombe Mwenyekiti wa Umoja wa umoja wa Afrika Mohamed Cheikh Rais wa Mautrania kuridhia uanzishwaji wa tume ilikukabiliana matatizo sugu barani Afrika" Alibainisha Luhaga Mpina.

Post a Comment