Na Magrethy Katengu--- Dar es salaam
Serikali imesema
itaendelea na jitihada za kuhakikisha inajenga vituo vingi vya afya na
kuboresha miundombinu ikiwemo vifaa tiba na usafiri ili kusaidia kila mtu
anapohitaji huduma kat za afya anahudumiwa vizuri na watoa huduma.
Ameyasema hayo leo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo Mai 17, 2024 katika hafla ya ugawaji bajaji 18 na vibao vya kupima Urefu watoto walio chini ya umri wa miaka mitano vifaa
hivuo ni kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa huduma na kutekeleza afua za
lishe.
Vipimo hivi vitakwenda kusaidia kujua mtoto kuanzia
anapozaliwa je yuko na uzito unaostahili ili aweze kusaidiwa kwenye eneo hilo
hivyo fedha zilizotengwa ni zaidi ya
shilingi milioni 300 ambazo zinaenda kwenye afua za lishe na miongoni mwa fedha
hizo milioni 22 zimekwenda kununua
vipimo hivi kwa ajili ya watoto"
amesema Mkuu wa Wilaya
Mpogolo amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM
imeahidi kuboresha huduma za Afya na moja ya maboresho ni eneo la ujenzi wa
miundombinu ambapo Mhe Rais Dkt Samia ametenga
zaidi ya Dolla bilioni 26 kuboresha miundombinu
katika halmashauri ya jiji la Ilala na
ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi
wa vituo vikubwa viwili vya afya cha
Mchikichini kinachogharimu kiasi cha fedha bilion 5 na kituo cha Mzinga mradi
wenye thamani ya bilioni 2.5 na na hadi
sasa kuna vituo vya afya zaidi ya 10 na
vipo katika hatua za mwisho kukamilika .
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Ilala Dkt Zaituni
Hamza amesema moja ya shughuli zao ni
kutekeleza vipaumbele muhimu vya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani
kuhakikisha huduma za afya zinatolewa vizuri
"Tulitengewa fedha na katika fedha hizo hivyo tumenunua
bajaji 18, ztakazo
tumika na watumishi ikiwemo 3kufutilia makuzi ya mtoto
nyumba kwa nyumba ,3 chanjo,3 shughuli za kutokomeza Malaria Nchini ,3ustawi wa
jamii '"amebainisha Dkt Zaituni
Aidha watumishi wote waliokabidhiwa vifaa hivyo wameombwa
kuvitunza vizuri na kuvitumia kwa mlengo uliokusudiwa.


Post a Comment