NEMC YATOA SIKU 90 KWA WAMILIKI WA VITUO VYA AFYA KUWEKA MIUNDOMBINU YA KUTEKETEZA TAKA.

......................

NA: Issah Mohamed –Dar es salaam.

EMAIL: issahmohamedtz@gmail.com

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira –NEMC, limetoa siku 90 kwa wamiliki wa vituo vya Afya na hospitali kuweka miundo mbinu ya kuteketeza taka zinazotokana na huduma za afya au kuwapa wakandarasi waliothibitishwa na sheria ili kuepuka kuhatarisha afya na mazingira kwa ujumla.

Tamko la baraza hilo limetolewa Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi uzingatiaji na ufuatiliaji sheria, Hamadi Taimur wakati akielezea tabia iliyoibuka hivi karibuni ya utupaji taka zitokanazo na huduma za afya mitaani.

Amesema baraza hilo linakemea vikali tabia hiyo ikiwemo wafanyabiashara wa huduma za afya kuwapa taka watu ambao hawajaidhinishwa kutoa huduma hiyo na hatimaye kuzitupa hovyo jambo ambalo ni hatari kwa afya na mazingira.

‘’Baraza linatoa siku tisini yaani miezi mitatu wote wenye zahanati,vituo vya Afya na Hospitali kuweka miundominu madhubuti ya kutekeza na kuhifadhi taka hizo la sivyo wenye maeneo hayo wanapaswa kuwapa taka hizo wakandari waliosajiliwa na wizara au –NEMC’’ Amesema Taimur.

Katika hatua nyingine Taimuru amesema baada ya muda huo kupita watafanya ukaguzi kwenye vituo vya afya kuona utekelezaji wa agizo hilo na wale ambao watakiuka watachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kusimamishwa kutoa huduma mpaka watakapotekeleza agizo hilo.

‘’Baraza pamoja na mamlaka nyingine husika tutafanya ukaguzi kuanzia vituo vya afya, Zahanati pamoja na Hospitali zote Nchini kwa kupitia kanda zetu na makao makuu ili kubaini wale wanaoendelea kukiuka agizo hilo na atakayebainikia tutamchukulia hatua za kisheria ikiwemo kusimamisha huduma zake; Ameongeza Taimur.

Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kifungu cha 137 pamoja na kanuni za usimamizi wa taka hatarishi kanuni ya 52 mpaka 58 inaelekeza utaratibu wa usimamizi wa taka zinazotokana na huduma za afya ambazo ni vifaa vyenye ncha kali ikiwemo viwembe na sindano.






0/Post a Comment/Comments