RADA TANO ZA HALI YA AHEWA ZAFUNGWA,NYINGINE KUKAMILIKA MWEZI NOVEMBA MWAKA HUU

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati akisoma bajeti ya Wizara yake bungeni jijini Dodoma leo Mei 6,2024Wakuu wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Uchukuzi wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, jijini Dodoma leo, Mei 6, 2024.

..............

Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekamilisha ufungaji wa rada za hali ya hewa katika mikoa ya Kigoma na Mbeya na kufikisha jumla ya rada tano za hali ya hewa nchini

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa wakati akisoma bajeti ya Wizara yake bungeni, ambapo ameeleza pia ujengwaji wa rada nyingine mbili unaendelea kiwandani nchini Marekani na inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2024.

Profesa Mbarawa amesema kuwa rada hizo zitafungwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Dodoma na hivyo kukamilisha lengo la muda mrefu la kuwa na rada saba za hali ya hewa nchini.

Aidha amesema kuwa TMA imeendelea kutoa utabiri wa kila siku wa siku kumi na wa muda  mrefu pamoja na tahadhari ya matukio ya hali mbaya ya hewa ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.

0/Post a Comment/Comments