..........
Na .Timothy Marko
RAIS wa Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua mpango mkakati wa Nishati safi ya kupikia.
Mpango huo ulianza November 2022 unalenga kuhamasisha Matumizi ya nishati safi na kuondokana matumizi ya nishati Chafu (Mkaa,pamoja nakuni)
Akizungumza katika uzinduzi huo Jijini Dar es salaam Rais Dk .Samia Suluhu Hassan amesema lengo la mpango huo nikutokomeza matumizi ya Nishati Chafu ifikapo 2034.
"Inakadiriwa Jumla hekta 4.69 za misitu hukatwa kutokana utafutaji wa Nishati, Takribani watanzania 33000 kwa mwaka hufariki kutokana Nishati Chafu"Alisema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aliongeza kuwa Azima ya Serikali ya Awamu ya Sita nikuo geza uelewa juu ya Matumizi ya nishati safi na kuondokana matumizi yanishati chafu.
"SERIKALI imelenga kuhamasisha matumizi ya Gesi ikiwemo Gesi ya lipa kadri unavyotumia,nakuhamasisha upandaji wa miti"Alisisitiza Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alisema kuwa Uzinduzi huo wanishati ya kupikia 2024-2030 ni moja ya mikakati ya kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya nchi na kuhamasisha Matumizi safi ya kupikia.
"Miongozo ya Sera na kanuni imewekwa katika kuratibu Matumizi yanishati bora yakupikia"Alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mazingira Dk.Suleman Jafo amesema takribani watu milion2.5 hufariki Dunia kutokana na kutumia nishati Chafu ya kupikia.
Alisema ifikapo 20 Mei mwaka huu taasisi zote zihamasishe matumizi ya nishati safi yakupikia.
"Takribani Magereza 126 Nilazima yatumie nishati safi yakupikia" Alisema Waziri wa Nchi,Mazingira Dk.Suleiman Jaffo.

Post a Comment