SHULE ZA SERIKALI BADO NI MKOMBOZI WA ELIMU NCHINI .



     Shule ya Mbezi na Ufundi Manispaa ya Ubungo

************

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Shule ya Msingi Mbezi na Ufundi , Manispaa ya Ubungo, Kata ya Mbezi , Ndugu Daniel Machage amesema kwamba michango yote kwa ajili ya mitihani ya mihura na Moko inafanywa baada ya kikao cha wazazi kuridhia kama muongozo wa wizara ya elimu na ufundi unavyotaka kwa kuwa Shule za serikali ni mkombozi wa  elimu hapa nchini. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake leo asubuhi jijini Dar es Salaam, Bw Machage amesema kwamba kila mwezi wa Juni huwa wanafanya kikao na wazazi shule hapo ili kupata maendeleo ya kitaaluma kwa maslahi mapana ya Watoto wa kitanzania.

“sio kweli kwamba mimi nakusanya michango kwa wanafunzi kupitia wazazi wao bila kufanya nao vikao Hapana huwa tunakuwa na vikao hapa tena safari hii nataka mje kwenye kikao , na naweka na (speakers) kubwa mpaka kule stendi ya magufuli wanasikia hii yote ni kwa manufaa ya hawa wananchi na Watoto wa  hapa mbezi,”amesema kwa msisitizo

Aliongeza kwamba ni kweli fedha kutoka serikali zinakuja kupitia Tamisemi kiasi cha shilingi 1.2 milioni kila mwezi ila ni kwa ajili ya ukarabati wa shule , miundombinu , vifaa na mambo ya michezo Pamoja na gharama zingine ila haitoshi kwa kweli lakini siwezi kukusanya fedha bila idhini ya wazazi , Mkurugenzi na kibali cha Mkuu wa Wilaya (DC)

“Katika hiyo fedha 1.2 millioni utoe 2% ili uweze kugharamia mitihani ya mihura, moko nay a kata kwa wanafunzi wasipoungua 2,532 na darasa la saba pekee ni wanafunzi 291 hii (capitation) ya serikali haiwezi kutosha ndugu zangu,”alisisitiza kwa sauti ya upole

Aliendelea kusema kwamba Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  ingawa hakutoa maandishi ila yatakuja amesema kwamba kwa madarasa ya mitihani kila wiki wanaweza kuchangia 1500 na kwa madarasa ambayo hayana mitihani kila mwezi 1000.

“Sasa sie hapa tunajibana bana kwa fedha ya madarasa ambao hawana mitihani tunakusanya kila mwezi tunagharamia mitihani ya kata hapa shule ya mbezi mitihani ya kata hatukusanyi michango kutoka kwa wazazi,’ alisema kwa kujiamini .

Aliendelea kusema kwamba shule za serikali ni mkombozi kwa watanzania wengi hapa nchini kwa sababu watu wanapata nafasi ya kusomesha Watoto wao kwa gharama ndogo na wanapata elimu nzuri.

Awali mwandishi wa habari hii alimtafuta mwalimu huyo mkuu kutoa ufafanuzi wa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya kukusanya michango kwa wanafunzi, kutumia lugha zisizo na staha kwa walimu na mahusiano mabaya na wenzake.

Akifafanua juu ya tuhuma hizo alisema kwamba sio kweli kwamba yeye anatumia lugha za mbaya ni kusimamia kanuni, sheria na taratibu za serikali katika kuhakikisha taaluma inapanda shule hapo.

“kama mimi ningekuwa na mahusiano mabaya na walimu wangu nisingeweza kupandisha kiwango cha ufaulu cha shule hii kwa sababu ufaulu unapanda kwa sasa shule hii ni ya 20 katia 80 katika wilaya ya Ubungo tunakwenda vizuri kwa kweli.

Kwa Upande wake, Afisa Elimu wa Wilaya ya Ubungo, Ndugu Denis Nyoni alisema kwamba michango yote inayokusanya shule lazima kuwa na vikao kati ya wazazi na uongozi wa shule na wazazi wanarishia kuchangia gharama za elimu hapa nchini.

“sikia ndugu yangu fedha za serikali zinakwenda kila mwezi ila pale ambapo hapakutosha wanaweza kukusanya michango kama waraka wa serikali unanyosema na kibali kinatoka kwa Mkuu wa Wilaya (DC) na si vinginevyo,”alisisitiza Ndugu Nyoni

Ndugu Nyoni aliongeza kwamba taratibu zote za serikali zinafuatwa na sio kweli kwamba Mwalimu Mkuu wa hapo mbezi anafanya kwa matakwa yake mengine watu wanakuwa na maslahi yao kwa kweli (interest zao) ila kama kuna tofauti naweza kufuatilia.

Kwa Upande Mratibu wa Elimu Kata ya Mbezi, Bi Suzana Massawe amesema kwamba upande hajawahi kupata malalamiko hayo ya ukusanyaji wa michango ua mitihani shuleni hapo kama yapo anafuatilia.

 Awali kulikuwa na tuhuma dhidi ya Mkuu huyo wa Shule ya Mbezi kwa anafanya unyanyasaji kwa walimu , kukusanya michango bila vikao na wazazi na kuendesha shule kinyume na matakwa ya serikali.

Taarifa za awali zilidai kwamba Mwalimu Mkuu huyo nim babe , ana kiburi , anatoa lugha zisizo na staha kwa walimu wa kike na kufanya matendo ambayo ni kinyume cha maadili kwa viongozi wa umma.

Mwisho .

 

0/Post a Comment/Comments