TANZANIA YA 97 DUNIANI KWA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

 

**************

Na.Timothy Marko 

Tanzania inashika nafasi ya 97Dunianikwa Mwaka 2024 ikilinganishwa na nafasi  143 Mwaka Jana ambapo kwa Mwaka huu Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa Kuzingatia Uhuru wa kupata taarifa  Barani Afrika ikilinganishwa nafasi ya 39 katika Upatikanaji wa taarifa na Uhuru wa kujieleza.

Akitoa tathimini hiyo kwa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi amesema kuwa  Katika kipindi cha Serikali ya Awamu yasita inayongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amesema katika kuzingatia  Uhuru wa Vyombo vya Habari Nchini Serikali imeweza kuyafungulia Magazeti Manne ambayo hapo Awali yalikuwa yamefungwa.

"RAIS wetu Dk. Samia Suluhu Hassan anaipenda Sekta ya Habari ,kabla ya uhuru tulikuwa na Magazeti kumi lakini sasa tuna Magazeti 400"Alisema Mkurugenzi wa idara Habari Maelezo  Mobhare Matinyi.

Mkurugenzi Matinyi aliongeza kuwa Nivyema vyombo vya Habari  vikazingatia Miko ya  tasnia ya Habari kwa kuzingatia Heshima ya  Utu wa binadamu kuwaUanzishwaTasisi ya Wanahabari kusini Mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-TAN) unalenga kujenga Uwezo wa Waandishi wa Habari hususan Magazeti na Radio.

"Hadi Sasa tuna Runinga za Mitandaoni zipatazo 300 na Radio 300 katika kutekeleza utekelezaji Uhuru wa vyombo vya Habari"Alisitiza Mobhare Matinyi.
Aidha,Mkurugenzi wa MISA -TAN  Elizabeth Riziki amesema katika Maadhimisho ya miaka 30 ya taasisi hiyo imekuwa ikiangazia uchechemuzi juu ya uhuru wa kujieleza na Uhuru wa vyombo vya Habari.
Alisema Wakati Taifa likielekea katika Uchaguzi Jumuhia hiyo imelenga kutoa Elimu ya  Uraia kwa kushirikiana wadau wa Maendeleo.
"Uongozi uliopo Umeruhusu Uhuru wa vyombo vya Habari lakiini vyombo vingi vya Habari vimekuwa vukikabiliwa na Rasmali fedha"Alisema Mkurugenzi wa Misa -Tan Elizabeth Riziki.


0/Post a Comment/Comments