TBS: MAADHIMISHO YA SIKU YA VIPIMO DUNIANI "TUNAPIMA LEO KWA UENDELEVU WA KESHO"




Shirika la Viwanga Tanzania (TBS) imeadhimisha siku ya vipimo Duniani Leo Tarehe 30 Mei, 2024 Mkoani Mbeya. Maadhimisho hayo ufanyika kila Mwezi wa Tano Tarehe 20 ya kila mwaka.

TBS kupitia maabara yake ya Metrolojia imepewa dhamana ya kutunza viwango vya vipimo kitaifa na kutoa unasabishaji wa vipimo, kuwakilisha nchi kimataifa katika masuala ya vipimo pamoja na kutoa mafunzo na Ushauri katika masuala yote ya Vipimo.

Mkurugenzi wa Upimaji na huduma za Metrolojia (TBS) Ndugu Ridhiwani RAMADHANI Matange Amesema " Ni ukweli usiopingika kwamba Elimu ya Metrolojia na huduma za ugezi ni nyenzo muhimu katika utoaji wa huduma Bora na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora ili kuimarisha biashara ndani na nje ya Nchi".

Pia amesema tunapoadhimisha siku hii ya Leo tunakumbushwa umuhimu wa vipimo sahihi katika maisha ya kila siku yanayomzunguka mwanadamu kama kauli mbiu yetu inavyosema " VIPIMO KWA UENDELEVU".

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TBS) Prof. Othman Chande Othman wakati wa maadhimisho hayo amesema " vipimo ni msingi wa Maendeleo. Vinatupatia takwimu na taarifa muhimu zinazohitajika ili kufanya maamuzi  sahihi, kuendeleza uvumbuzi, na hatimaye kuhakikisha Maendeleo endelevu. Mfano kupima ubora wa vifaa vinavyotumika  kwa ajili ya kujenga miundombinu kama madaraja na barabara, kupima ubora wa maji tunayotumia na kutathimini ubora wa vifaa vinavyotumika katika kutoa tathimini ya Hali ya hewa.

Pia Prof. Othman Chande Othman amewakumbusha washiriki wote katika maadhimisho haya kutumia  maadhimisho haya kama Jukwaa la kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa Vipimo sahihi katika kushughulikia changamoto za kijamii, kimazingira na kiuchumi na kusisitiza matumizi ya vipimo sahihi kwa UENDELEVU.

0/Post a Comment/Comments