***************
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Kuna uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.
Aidha, kutokana na umbali
kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja
katika kusababisha ongezeko la mvua nchini.
Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi
makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.
Aidha Watumiaji wa bahari
na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa
za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na
miongozo ya wataalam wa kisekta.
TMA imesema inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga
hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa
taarifa kila inapobidi.

Post a Comment