TMDA YAWATUNZA WANAHABARI WANNE KWA UANDISHI BORA

******

Na Tausi Mbowe, Iringa

Ni furaha kwa waandishi wa habari wanne kati ya wengi waliwasilisha kazi zao kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), baada ya kuibuka washindi. 

Waandishi hao wameibuka kidedea katika shindano linalloratibiwa na Mamlaka hiyo kila mwaka kwa kuandika habari bora za afya. 

Veronica Mrema ndiye aliyeibuka mshindi wa jumla huku, Andrew Chale, Penina Malundo na Madina Mohamed. 

Washindi hao wa mwaka 2024 walitangazwa mapema wiki hii katika tukio la kihistoria wakati wa Kikao kazi cha mwaka kilichohusisha Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) na wadau wa vyombo vya habari kilichofanyika Mei 16, 2024 mkoani Iringa. 

Washindi hao wa kihistoria walichaguliwa kwa kuzingatia vigezo mahususi ili kuwapata waandishi wa habari waliojitolea muda na juhudi zao kuandika mada zinazoelimisha umma kuhusu kazi na majukumu ya TMDA. 

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwatunza waandishi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo aliwapongeza washindi kwa kujitolea kwao na kuwataka kuendelea kuandaa na kuchapita habari za Mamlaka hiyo zenye mahudhui ya udhibiti wa bidhaa mwakani. 

"Tunawaomba muendekee kuandika juu ya masuala yanayohudu udhibiti wa bidhaa, ufanisi, ubora na usalama wa bidhaa tiba ili wanannchi wafahafu zaidi majukumu yetu na kujilinda dhidi ya bidhaa zisizofaa kwa matumizi, " alisisitiza Dk Fimbo. 

Awali Meneja Mawasiliano na Mawasiliano kwa Umma, Gaudensia Simwanza katika mada yake alienza mchakato wa kuwpaata washindi hao ulihusisha mchujo mkali na kusisitiza kwamba washindi waliopatikana waliwasilisha kazi zao TMDA kwa ajili ya kushindanishwa. 

Simwanza aliwahimiza waandishi wa habari nchini kujitokeza kwa wingi katika kinyang'anyiro kama hiko mwakani zitakapotangazwa tena. 

Washindi hao walitunukiwa kikombe kama ishara ya pongezi pamoja na zawadi ya fedha tasilimu. 

Kwa mujibu wa Simwanza, zawadi hizo ni motisha ili kuwashawishi waandishi wengi zaidi kushiriki katika tuzo hizo kwa siku za usoni.


 




0/Post a Comment/Comments