TRA YA KUSANYA SHILINGI TRION 24 MWAKA WAFEDHA 2022/2023.





.........

Timothy Marko

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imesema katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2022/23 imeweza kukusanya Shilingir  trioni 24 ikilinganishwa  nakipindi cha Mwaka 2021 /2022  Cha Shilingi trioni 18 .

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar  es  Salaam Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipakodi wa Mamlaka hiyo Hudson Kamoga amesema Ukuaji wa Makusanyo hayo yametokana najitiahada mbalimbali  za Utoaji Elimu kwa Mlipa kodi ikiwemo Ulipaji kodi kwa hiyari sambamba na Uanzishwaji wa Mfumo mpya wa Ukusanyaji kodi (ETS) Eletronic Stamp  .

 "Matumizi ya Mfumo Umetokana sheria yaBunge ya Ukusanyaji Mapato kietroniki ya Mwaka 2022,kutokana na Mfumo huo umewezesha Makusanyo ya kodi ya Shilingi trioni 11 Mara baada yakuanzishwa Mfumo huu"Alisema Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipakodi Hudson Kamoga.

MWENYEKITI wa Jumuhia ya Waandishi wa HabariMitandaoni Nchini(JUMIKITA) Shabani Matwebe amesema kuwa Nimuhimu Kwa Mamlaka hiyo kuweza kutumia Waandishi wa Habari wa Mitandaoni Juu ya Umuhimu wa Wananchi kuweza kudai Risiti Mara baada ya kununua Bidhaa ili kuchochea Maendeleo ya Nchi.

"Kudai Risiti  ni Jambo la Msingi ,kwani Suala hili niJambo la kimaendeleo,Jambo la Msingi Ni kumsaidia Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan Kwa Sisi waandishi  Kuhamasisha Wananchi kulipa kodi na kudai Risiti Marabaada yakufanya Manununuzi."Alisema Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe.

0/Post a Comment/Comments