Katibu wa Kamati ya Tuzo za KRMA III Stellah Kisinga (kushoto) akiendesha kikao ambacho kimewakutanisha wanamuziki wa wa Reggae katika Ofisi za Taasisi ya sanaa ya Kukayemoto Culture Center zilizopo Ubungo jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kamanda ya Maandalizi ya Tuzo za KRMA III na Mwanamuziki wa Reggae Ras Nono wakimsikiliza Mwakilishi Mratibu Wa KMCC Diana Martin kwenye Kikao na wanamuziki kilichofanyika katika Ofisi za Taasisi ya sanaa ya Kukayemoto Culture Center zilizopo Ubungo jijini Dar es salaam................
"Wanamuziki tumieni barua pepe ya krmaiiireggaeawards@gmail.com kutuma kazi zenu"
NA Musabhai
Wanamuziki wa Reggae nchini wameendelea kusisitizwa kutumia fursa ya kushiriki Tuzo za KRMA III Ili kuweza kujipatia fursa mbalimbali ikiwemo kupata zawadi na kufanya ziara nje ya nchi.
Hayo yamejiri mwishoni mwa wiki katika Ofisi za Taasisi ya Kukaye Moto Culture Center jijini Dar es salaam wakati Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Kukayemoto Reggae Music Awards awamu ya Tatu (KRMA III ) ilipowakutanisha wanamuziki mbalimbali wa muziki huo ili kujadili namna ya kushiriki katika mchakato huo ambao kilele chake usiku wa Tuzo ni Tar 30/6/2024.
Akifungua kikao Hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za KRMA III Innocent Nganyagwa maarufu Ras Inno amewasisitiza wasanii hao waliojitokea katika kikao hicho kuwa ni vyema kwa muda huu uliosalia wanakatumia fursa hiyo kuhakikisha wanatuma kazi zao ili ziweze kuingia kwenye mchakato.
"Katika mchakato huu umezingatia zaidi ya vipengele 30 vitahusika ambapo pia utafanyika uchakataji wa kazi pamoja na upatikanaji wa wateule"Ras Nganyagwa
Kwa upande wake Katibu wa Tuzo za KRMA III Stellah Kisinga amesema kuwa katika mchakato huo mtu anapofanya vizuri lazima apewe Tuzo hivyo wanaendelea kuwafungulia milango wasanii wanaoufanya Muziki huu kujitokeza kwa wingi kushiriki.
'Kwa mwanamuziki ambaye utashiriki katika Tuzo hizi tuma kazi na taarifa zako kupitia email ya krmaiiireggaeawards@gmail.com Ili nyimbo zako ziweze kuingia katika mchakato"amesema Kisinga
Mwakilishi Mratibu Wa KMCC Diana Martin amesema kuwa utoaji wa Tuzo ni moja ya mradi ambao unafanya na Kukayemoto Culture Center ambapo pia chimbuko lake lilianzia Ujerumani na Iringa nchini Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya wanamuziki,Mwanamuziki Ras Nono anasema "baada ya kuona taarifa kuhusu kikao cha Reggae nimefurahi sana na hivyo nikaamua kujitokeza ili kuweza kushiriki katika kikao hiki"
Ras Nono amesema kuwa kutokana na baadhi ya wanamuziki kukutana na changamoto katika tasnia yao imepelekea kutoshiriki katika baadhi ya shughuli za kirasta na reggae.





Post a Comment