...........
Mkaguzi Kata ya Kiutu Wilayani Arumeru Mkoani Arusha amewataka wanafunzi kutambua kuwa baada ya kumaliza elimu yao ya kidato cha Sita sio Mwisho wa Masomo huku akiwasihi kutojihusisha na makundi ambayo yatawapotosha na kuharibu dira ya maisha yao.
Kauli hiyo ameitoa Mkaguzi Kata ya Kiutu Mkaguzi wa Polisi INSP Tunu Pingu baada ya kukutana na wanafunzi wa Sekondari ya Enaboishu waliohitimu Elimu yao ya kidato cha Sita ambapo amewambia kuwa dhamira ya wazazi na Serikali nikuona vijana wanaomaliza elimu zao mbalimbali wanalisaidia Taifa kukua kiuchumi na maendeleo yao binafsi.
Pia amewataka kuwa mabalozi wa kupinga vitendo vyote viovu katika Jamii ili kuwa na Jamii yenye kuchukia uhalifu na vitendo vya kikatili.
Sambamba na hayo amewataka kutambua kuwa bado wanasafari ndefu katika Masomo ambapo amewataka kutunza afya zao kutojihusisha na uasherati na matumizi ya dawa za kulevya ambapo amebainisha kuwa zitakatisha ndoto zao katika maisha.
Mwisho aliwaambia wanafunzi hao kuwa endapo wanatamani kuwa kama yeye ni vyema wajibiidishe katika masomo ambayo yanaendelea baada ya elimu ya sekondari.

Post a Comment