..........,.......
WIZARA ya Ardhi imejipanga kimkakati Katika kufanikisha zoezi la ukwamuaji kwa kuendeleza maeneo yaliyoachwa na wakandarasi wakati wa upimaji Ardhi maeneo mbalimbali ya nchi
Akizungumza na wanakamati wa Jimbo la ukonga Jijini Dar Es Salaam Afisa Mipango Miji mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi John Mbembela amesema ukosefu wa elimu ya milki kwa Wananchi na wanakamati wa zoezi la Urasimishaji ndio chanzo Cha kukwama kwa upimaji maeneo mbalimbali nchini
Mbembela amesema majukumu ya kamati za Urasimishaji Katika mitaa ni kushiriki Katika upangaji, kuratibu shughuli za Urasimishaji na kuhamasisha Wananchi kulipia gharama za upimaji kwa Kushirikiana na makampuni ya upimaji yaliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria
Kikao kilishirikisha kamati kutoka mitaa ya Kitunda, Kipawa, Kivule, Kipunguni na Msongola ambapo wajumbe walishiriki kupata Elimu ya namna bora kushiriki Katika zoezi la ukwamuaji na kutatua changamoto zilizojitokezeza kwenye upimaji Makazi Uliofanyika awali, kamati zimetakiwa kufanya kazi kizalendo, Weredi na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa
Mbembela amesisitiza kuwa kamati hazitakiwi kushiriki Katika upimaji kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia isiyo halali kutoka kwa Wananchi, kwani kufanya hivyo ni kukiuka mwongozo wa zoezi la Urasimishaji, amesema kila mwanakamati anapaswa kufuata taratibu ziliwekwa kisheria ili Kuepuka migongano kimaslahi na kuongeza migogoro zaidi badala ya kutatua na kusababisha Wananchi kulalamikia serikali
Kwa upande wa wanakamati wameishukuru serikali kwa kuanzisha zoezi hili muhimu na kuahidi Kushirikiana na Serikali Katika kukwamua upimaji uliokwama kwa kuendelea kutoa Elimu zaidi kwa Wananchi, Letisia John kutoka Mtaa wa Machimbo amesema Elimu ya kupanga na kupima kwa pamoja itasaidia Kupunguza maswali magumu kutoka kwa Wananchi, na kutadaidia kuongeza kasi ya Wananchi kuchangia fedha kwa ajili ya kuwezesha upimaji kuwa mwepesi zaidi
Naye Peter Fanuel mwanakamati kutoka Mbondole amesisitiza uharaka wa kuchakata nyaraka na michoro kwenye ofisi za Ardhi ili kuweka wepesi wa nyaraka kama vile michoro ya mipango miji pindi zinapohitajika
Zoezi hilo la ukwamuaji litaendelea maeneo mbalimbali Jijini Dar Es Salaam na Wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kutoa ushirikiano kwenye kuonesha mipaka yao pamoja na kuchangia fedha kwa ajili ya gharama za upimaji Ardhi





Post a Comment