Dar es Salaam. Maeneo tofauti nchini Tanzania yanashuhudia mvua kubwa ambazo sio tu zinaathiri miundombinu na kuhatarisha usalama wa maisha ya watu bali pia inaweza kuwa hata kwa vifaa vya umeme nyumbani.
Watu wengi huingia hasara wakati vyombo vyao vya umeme walivyovinunua kwa gharama kubwa kuharibika kutokana na hitilafu za umeme. Mara nyingi matukio ya aina haya yanaweza kuzuilika endapo tahadhari zikichukuliwa mapema.
Akizungumzia kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia, Meneja wa Bidhaa za Kieletroniki wa Samsung Tanzania, Bw. Evans Songa ametolea ufafanuzi maswali ya msingi ambayo wateja wengi wamekuwa nayo hususani kwa wanaoishi na familia au wenyewe, ili kuhakikisha usalama wa vyombo vya umeme nyumbani.
Madhara ya kutumia vyombo vya umeme mikono ikiwa imelowana ni pamoja na mtumiaji kupigwa shoti ya umeme.
Swali: Nini kinashauriwa baada ya kumaliza matumizi ya vyombo vya umeme nyumbani?
Jibu: Kuna baadhi ya watu wana kawaida ya kuacha vyombo vyao katika soketi za umeme baada ya kumaliza matumizi.
Mbaya zaidi wengine husahau hata kuzima kabisa kutokana na vifaa vingi vya siku hizi ni automatic hivyo kujizima vyenyewe mara tu vikimaliza kazi iliyokusudiwa. Tabia hii inaongeza hatari ya chombo kuharibika au kuungua endapo kutatokea shoti ya umeme.
Hii itakulinda hata endapo utatoka nyumbani kwako kwa dharura au kuendelea shughuli zingine.
Sidhani kama utafurahi siku ambayo una uhitaji zaidi wa chombo chako na kugundua kuwa hakifanyi kazi aidha kutokana na kutokitunza au kujaribu kama kinafanya kazi mara kwa mara.
Sio kampuni zote zinatoa warantii kwa bidhaa wanazouza kwa wateja wake.
Kigezo muhimu cha kupata warantii ni kununua bidhaa kutoka kwa mawakala wa bidhaa waliohakikiwa pamoja na kuwa na kadi ya warantii kwa bidhaa za nyumbani.
Kuongezeka kwa makampuni ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa hivyo pia kumepelekea urahisi na unafuu wa upatikanaji wake.
Bila kusahau kuongezeka kwa matumizi ya umeme nchini kote ambayo yanahamasisha watu kubadilika kuendana na wakati.

.jpg)

Post a Comment