.................
MRATIBU wa zoezi la Ukwamuaji mkoa wa Dar Es Salaam na Afisa Mipango Miji mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Paul John Mbembela amewataka Wananchi kutumia fursa ya zoezi la ukwamuaji kama njia ya kumaliza changamoto zilizojitokeza wakati wa zoezi la Urasimishaji nchini
Ameyazungumza hayo Katika Manispaa ya Temeke, Jijini Dar Es Salaam wakati wa semina elekezi kwa kamati za Urasimishaji Ardhi ili kutoa Elimu na Kuwajengea uwezo wanakamati ili waweze kumaliza kero watakazokutana nazo pindi wawapo kwenye mradi wa Urasimishaji
Mbembela amesema zipo zipo kasoro zilizojitokeza wakati wa upimaji wa vipande vya Ardhi Katika maeneo mbalimbali hususani Jiji la Dar Es Salaam, amesema Wizara imelichukua jukumu hili kufuatia kusuasusa kwa baadhi ya makampuni ya Urasimishaji na kupelekea malalamiko mengi kutoka kwa Wananchi wakidai Hati milki
Baadhi ya makampuni yalikosa sifa ya kuchukua kazi za kupima vipande vya Ardhi na kukosa ushirikiano wa karibu na Wananchi au uadirifu wa kazi waliyopewa kwa mujibu wa mikataba iliyopo
Jambo lingine liliotajwa Katika kikao hicho ni kamati za Urasimishaji kukiuka mwongozo uliowekwa ikiwa ni pamoja na uteuzi wa wajumbe, kasoro nyingine ni baadhi ya wanakamati kuficha michoro au namba za ploti (Plot number) ili kujipatia fedha zisizo halali kutoka kwa wananchi
Baadhi ya wananchi kushindwa kulipia fedha za upimaji kwa wakati, pia baadhi ya kamati kukosa Weredi na kuweka maslahi binafsi na kuzorotesha kazi iliyopo au kushindwa kumalizia kazi ya kupima viwanja kama ilivyokusudiwa
Kamati za Urasimishaji zimeshauriwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kusababisha ugumu Katika kumaliza kazi kufuatana na mkataba uliopo
Wenye makampuni kushindwa kulipia gharama za ofisi na kusababisha ofisi kufungwa na michoro kubaki ndani kutokana na madeni Makubwa
Makampuni kupeleka wataalamu wachache na wasio na sifa, kampuni kuchukua kazi kubwa kuliko uwezo, na kusababisha mlundikano wa kazi zilizochukuliwa Katika mitaa
Ulinzi Kwenye wa nyaraka na alama za upimaji unaopelekea Wananchi kukosa taarifa Sahihi za eneo lao na kusababisha migogoro isiyo na ulazima
Kukosekana kwa Elimu kumetajwa na wanakamati ambao wanaunda kamati hizo bila kufuata mwongozo kwa kuteua watu wasio na sifa, sehemu zingine wenyeviti walishindwa kujua mipaka ya majukumu yao na kusababisha mwingiliano baina ya kamati na makampuni ya upimaji
Aidha, baadhi ya wanakamati Wakiongea na gazeti hili wameipongeza serikali kwa kutafuta fedha kutoka kwa wahisani Benki ya Dunia ili ukwamuaji ufanyike na kurahisisha Wananchi kupata Hati zao kwa wakati
Simba Athumani mkazi amesema uwepo wa utoaji wa elimu kutasaidia wanachi kukwamuliwa na kupata Hati kwa haraka na wepesi





Post a Comment