AGAPE BENDI KUNOGESHA TWENZETU KWA YESU.

******

Timothy Marko

BENDI ya Agape Gospel inatarajiwa kunogesha Tamasha Twenzetu kwa yesu Katika Viwanja vya Tanganyika  Peackers Juni 15 Mwaka huu jijini Dar es Salam .

Akizingumza na Waandishi wa Habari jijini Naibu KatibuMkuu Dayosisi Mashariki na Pwani (KKKT) Willbroad Mastai amesema Bendi hiyo inayo sifika na Wimbo wa Hallo mbiguni, inatarajia kunogesha tamasha twenzetu kwa yesu ikiwa na lengo la kuwa kutanisha Vijana waweze kumtumikia Mungu na kuepukana na Uovu.

"Neno la Mungu linasema Hutuponya nakutoa katika Maangamizo yote,Twenzetu kwa yesu tuna kuja na ujumbe Uwe nuru katika Maisha yako"Alisema Naibu Katibu Mkuu DMP Willbrod Mastai.

Willbrod Mastai aliongeza kuwa sambamba na Bendi hiyo Waimbaji wengine nipamoja Nakibonge wa yesu.

Alisisitiza kuwa katika Tamasha hilo vijana wanaotarajiwa kuhudhuria tamasha hilo 30,000 ambapo Dhumuni la tamasha hilo nikuwabadilisha Vijana kitabia kupitia Neno la Mungu.

"Kupitia Utumishi wa Neno la Mungu tunategemea Kumpata kijana anayejiepusha na uovu"Alisisitiza Wibrod Mastai.

0/Post a Comment/Comments