Timothy Marko
KATIKA kuhakikisha Mtanzania na Mteja Anamiliki Gari la Ndoto yake,BENKI ya ABSA imenzisha Mkopo Maalum wa kumiliki Gari la ndoto yake ijulikanayo "Miliki Gari ya Ndoto yako".
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Mkuu wa wa Mkuu wa kitengo Cha Wateja Binafsi wa Benki ya ABSA Lilian Ndabu amesema kuwa Benki hiyo imekuja na Mkopo huo wa Gari ili kumuwezesha Mteja wa Benki hiyo kumiliki Gari ya ndoto yake.
"Tunamuwezesha mteja kupata Mkopo Gari ya Ndoto yake kuanzia mkopo wa Shilingi milioni 30 hadi milioni 500 kwa kipindi cha Miaka mitano"Alisema Mkuu wa kitengo cha Wateja binafsi Lilian Ndabu.
Ndabu aliongeza kuwa mteja atanza kulitumia Gari huku akilipa Mkopo wake kidogo kidogo.
Alisisitiza kuwa Mkopo Unajumuisha Mkopo wa Magari yalitumika kwa Asilimia kumi huku Mkopo wa Magari yaliyotumika aslimia 20.
Kwa Upande wake Mkuu wa kitengo cha Mikopo wa Benki ya ABSA Patricia Nguma amesema Katika kuhakikisha Mteja wa Benki hiyo anufaika imekuja na mkopo wa Gari ilikuendana na matakwa ya soko.
Alisema Mkopo kwa Magari yaliyotumia niAsilimia 15 Wakati mikopo ya Gari jipya ni Riba ya Asilimia Asilimia 10.

Post a Comment