BENKI SELCOM MICROFINANCE YATENGA TRIONI 1.6 KWA WAJASILIMALI.

*********


Timothy Marko.

KATIKA kuhakikisha Wajasiliamali wa kati na wa chini wanawezeshwa kiuchumi ikiwemo kukuza Biashara zao kupitia Mikopo,Benki ya Selcom Microfinance Benki imetenga Shilingi trion1.6 ilikuwawezesha wajasimali wakati na wachini.

Akizungumza katika Uzinduzi  wa Benki ya Selcom Microfinance Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo jijini Dar es Salaam Julias Ruwaichi amesema zaidi ya vijana wakiwemo wakulima 2000,00 na wafanyabishara wameweza kupatiwa mikopo kwa kipindi cha Mwezi Mei.

"Mtaji wa Benki umefikia Shilingi Bilioni 8.6 baada ya miwili ijayo tunalenga kukuza mtaji hadi kufikia bilioni 20"Alisema Mkurugenzi Julias Rwaichi.

Rwaichi aliongeza kuwa tayari imeshafungua matawi mbalimbali katika mikoa ya Mbeya ,Iringa,Pamoja Dar es Salaam.

Alisisitiza kuwa Riba ya Benki hiyo ni Asilimia 2 hadi 4.8kutokana aina yamkopo yamteja atakayo chukua .

"Sekta ya kibenki zimekuwa zikaguliwa na kutathiminiwa "Alibaisha  Afisa Mtendaji Mkuu Sellcom MicroFinance Benki Julias Rwaichi.

 

0/Post a Comment/Comments