BODI YA MKOPO YA ELIMU YA JUU WAFUNGUA DIRISHA,DKT KIWIA AWAASA WAOMBAJI


 ***************

BODI ya Mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini(HESLB),imetangaza kufunguliwa dirisha la kuomba mkopo kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo 2024/2025 huku waombaji wametakiwa kusoma mwongozo kabla ya kuomba.

Akizungumza na Waandishi mapema leo Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji(HESLB),Dkt Bill Kiwia,amesema baada ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda kuzindua miongozo tarehe 27 Mei,2024 waliiweka miongozo hiyo kwenye tovuti ya Bodi ya Mkopo ambayo Www.heslb.go tz.

"Kwa mwaka wa masomo 2024/2025 dirisha la kuomba muopo kwa njia ya mtandao lipo wazi kwa siku 90 kuanzia Juni 1 hadi Agoust 31,2024"Amesema Dkt Kiwia,

Hata hivyo,Dkt Kiwia amesema muda wa siku tisini unatosha kwa waombaji na watanatakita kuandaa nyaraka muhimu,na itachukua dakika 40 kukamilisha maombi yake kwa njia ya Mtandao.

"Tunasisitiza waombaji kuzingatia muda uliotolewa kwa kuwa hatutarajii kuongezwa baada ya Agost 31,2024"Amesema.

Dkt Kiwia,kwa mwaka wa fedha 2024/2025,Serikali imetenga bilioni 787 kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 250,000,idadi hii imeongezeka kutoka wanafunzi 224,056 mwaka 2023/2024 ongezeko la jumla wanafunzi 25,944.

0/Post a Comment/Comments