DKT SAMIA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA HAYATI BENJAMINI MKAPA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini William Mkapa Foundation Dkt Ellen Senkoro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati Benjamini Mkapa yanayotarajiwa kufanyika July  31mwaka huu.Mwakilishi Wizara ya Afya Asnath Matunga akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati Benjamini Mkapa yanayotarajiwa kufanyika July  31mwaka huu.
Mkurugenzi wa Program na Ukuaji wa Kitaasisi  Mkapa Foundation Rahel Sheiza akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati Benjamini Mkapa yanayotarajiwa kufanyika July  31mwaka huu.Baadhi ya wanahabari wakifuatilia na kuchukua matukio katika mkutano baina yao na Viongozi wa taasisi ya Taasisi ya Benjamini William Mkapa Foundation.

...................

NA MUSSA KHALID 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  maadhimisho ya kumbukizi ya Hayati Benjamini Mkapa July  31 mwaka huu ili kuangazia maono na kazi mbalimbali za Hayati Benjamin Mkapa katika kuongeza chachu ya maendeleo ya ndani ya nchi, kwa kutumia raslimali, sera na mifumo ya ndani katika kuleta maendeleo. 

Imeelezwa Pia Takriban washiriki zaidi ya mia tano wanategemewa kuhudhuria Kongamano la rasilimali watu katika sekta ya afya,huku viongozi wapatao 600 wakitegemewa kushiriki katika kilele cha Kumbukizi ya Hayati Benjamini Mkapa inayotayajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu. 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamini William Mkapa Foundation Dkt Ellen Senkoro amesema kumbukizi hiyo itaanza kwa kongamano la Rasilimali Watu wa Sekta ya Afya litakaloshirikisha wadau wakiwemo wataalam wa afya ngazi zote na kufanyika julai 29 hadi 30 2024. 

Kumbukizi hii ya Hayati Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ni ya tatu kufanyika tangu kufariki kwake 23 Julai, 2020. Kumbukizi ya kwanza ilifanyika Julai 2021 jijini Dar es Salaam, na ya pili ilifanyika Julai 2022, Zanzibar. Aidha Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation iliamua kufanyika kwa kumbukizi kama hizi kila baada ya mwaka mmoja, na hivyo kupelekea kumbukizi ya tatu kufanyika  mwaka huu 2024, mwezi Julai”amesema Dkt Senkoro

Amesema kuwa Kongamano hilo litawaleta pamoja wadau mbalimbali kutoka Serikali, Wadau wa maendeleo, sekta binafsi, Vyuo Vikuu, wataalamu wa sekta ya afya, pamoja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambapo lengo kuu ni kubadilishana uzoefu, maarifa, kubaini fursa za masomo ya kujiendeleza na ajira mbalimbali kwa wataalam wa afya, na pia kupendekeza mikakati ya pamoja ya kupunguza changamoto za rasilimali watu katika sekta ya afya nchini.

Awali akizungumza Mwakilishi Wizara ya Afya Asnath Matunga amesema kuwa wadau wa Mkapa Foundation wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano na serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na stahiki ikiwemo eneo la ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Program na Ukuaji wa Kitaasisi  Mkapa Foundation Rahel Sheiza amesema kuwa taasisi hiyo  imekuwa ikitekeleza miradi ya Afya Nchini kuanzia ngazi ya Taifa hadi kwenye jamii Tanzania Bara na Zanzibar na kwa miaka 18 Mkapa Foundation imekuwa ikitekeleza afua za kuimarisha mifumo ya sekta ya afya ndani ya vituo vya kutolea huduma za afya na kwenye jamii.

Kumbukizi hiyo yenye jina la Mkapa Legacy Summit linalotarajiwa kufanyika Jijini Dar Es Salaam linategewa kufanyika kwa siku tatu mfululizo kuanzi jula 29 hadi 31 2024 ambapo kauli mbiu ni kuchagiza Uendelevu wa ndani kuelekea upeo mpya.

0/Post a Comment/Comments