Makubaliano hayo
yamefanyika katika hafla fupi kwenye Ofisi za FCC Leo Juni 5, 2024 Jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza na waandishi
wa Habari muda mfupi kabla ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa FCC,
William Erio, amesema lengo la kusaini makubaliano hayo ni kuhakikisha kila
mmoja anatekeleza majukumu yake kwa ufanisi kukuza viwanda na kudhibiti bidhaa
bandia.
“Kusainiwa wa makubaliano haya kutawezesha
kufikia malengo ya serikali ya Rais Dk.Samia ya kukuza uchumi kupitia sekta ya
viwanda.Mahusiano haya yatahusu namna bora ya kubadilishana taarifa hususan
utekelezaji wa sheria mbili ambazo FCC tunazisimamia ikiwemo ya Ushindani na ya
alama au nembo ya bidhaa zinazowahusu wenye viwanda,” amesema.
Amesema katika majukumu ya CTI
kupitia sera na dira zao zinaonyesha ambavyo wanalenga kulinda mazingira mazuri
ya kufanya biashara nchini kwa wenye viwanda kufikia matarajio yao na kukuza
uchumi wa viwanda.
Aidha Erio, amesema wanaendelea
kulinda na kushabihisha ushindani, hivyo wanahakikisha wanadhibiti vitu ambavyo
vinaweza kuathiri wawekezaji hao ikiwemo ukiukaji wa sheria na makubaliano
kuhakikisha havifanyiki.
Akielezea kuhusu sheria ya
bidhaa bandia amesema, inazuia kupitia mipaka ya nchi na kutozalishwa nchini,
ndiyo maana wamesaini makubaliano hayo kuhakikisha wanalinda uzalishaji huo
wenye tija katika kukuza ajira, fursa ya uchaguzi wa bidhaa na kukuza uchumi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye viwanda Nchini (CTI), Mhandisi Leodgar Tenga, ameipongeza FCC kwa kufanikisha kusainiwa kwa makubaliano hayo yanayotokana na ushirikiano mzuri wa Taasisi hizo mbili.



Post a Comment