Na Tausi Mbowe
Ili kuhakikisha usambazaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi unakuwa salama na viwango vya juiu Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa jukumu hilo kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA).
Mamlaka hayo si tu inahakikisha kazi hiyo inafanyika bali inazingatia viwango vya ubora vya utoaji wa huduma za afya.
Hivi karibuni TMDA ilifanyika ukaguzi wa kina wa ufuatiliaji wa hali ya usambazaji wa vifaa tiba na vitendanishi vinavyoingizwa nchini kwa vibali maalum.
Katika ukaguzi huo ulifanywa kati ya Mei 29 na Juni 2023 ulilenga kuhakilisha usambazaji sahihi wa vifaa katika soko kwa ajili ya biashara bila uchepushwaji, hasa vile vinavyoingizwa nchini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kama misaada.
Matokeo ya ukaguzi huo yaliwasilishwa kwa Mkurugenzi wa Vifaa Tiba na Uchunguzi wa TMDA, Kisa Mwamwitwa.
Ripoti hiyo iliwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mkoani Morogoro Septemba 9, 2023.
Ukaguzi huo ulitoa picha ya usambazaji wa bidhaa hizo.
Akizungumza mara baada ya kupokea ripoti ya ukaguzi huo mkurugenzi Kisa alisema asilimia 77 ya vifaa vya matibabu na uchunguzi viliingizwa nchini kwa vibali maalum vilifika mahali vilipokisudiwa.
Hata hivyo, ukaguzi huo uliibua hoja ya kuhusu vifaaa 311 vinavyojumuisha asilimia 23 ya jumla ambavyo havikuwa na stakabadhi na nyaraka zenye kumbukumbu za matumizi ya vifaa husika katika maeneo waliyopangiwa.
Mkurugenzi Kisa alisema kuhusu utofauti wa vifaa tiba 311 ambavyo havikukutwa kwenye vituo vilivyopelekwa wala nyaraka zilizohitajika, mamlaka ilitoa maagizo kwa waagizaji kutoa taarifa za kina kuhusu upotevu wa bidhaa hizo ndani ya muda ulioelekezwa.
Alisema ukaguzo huo ulilenga mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Mwanza, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Singida, Dodoma, Mbeya ambayo ina idadi kubwa ya vibali maalum ya kuingiza bidhaa nchini vilivyotolewa kwa mwaka mmoja kati ya January 2022 na February 2023.
Alisema katika ukaguzi huo jumla ya vibali maalumu 1558 vilitolewa katika kipindi hicho kwa ajili ya matumizi ya hospitali na vituo vya utafiti kama misaada.
Alieema kati ya vibali 788 ambavyo ni asilimia 50 vilifanyiwa ukaguzi na kubainisha kuwa vibali 464 sawa na asilimia 59 vilifanyiwa utafiti wa kina.



Post a Comment