******
Korea Kusini leo ni mwenyeji wa mkutano wa
kilele na viongozi wa kiafrika ambao wamewakilishwa na wajumbe kutoka nchi 48
wakiwamo wakuu wa nchi wapatao 30.
Alipokuwa
akihutubia mkutano huo mjini Seoul, Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol amesema
nchi yakeitazidisha misaada ya maendeleo
barani Afrika hadi karibu dola bilioni 10 ifikapo mwaka 2030 na
kwamba watatanua ushirikiano wa kina hasa katika sekta muhimu za madini na
teknolojia.
Baada ya mkutano huo Yoon na mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika, Rais wa Mauritania Mohamed Ould El-Ghazouani wanatarajiwa
kutoa taarifa ya pamoja.
Hapo kesho, wakuu wa biashara wa Korea
Kusini wataendesha mkutano wa kilele wa biashara utakaojikita katika masuala ya
uwekezaji, maendeleo ya viwanda na usalama wa chakula.
cc DWkiswahili
Post a Comment