Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4, 2024 jijini
Dar es Salaam, Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Lawrence Mafuru
amesema kongamano hilo linalenga la kukusanya maoni na kutoa elimu kuhusu
Tanzania tuitakayo ifikapo 2050.
Amesema kuwa ushiriki wa utoaji wa maoni hayo unaweza kuwa
wa aina nyingi ukiwa ni pamoja na kutuma ujumbe mfupi wa simu,majukwaa ya umma,
tafiti, mijadala ya mitandao ya kijamii na mikutano ya kijamii.
“Kongamano hili ni kubwa na la kwanza kufanyika, hivyo
uhamasishaji wa kongamano letu la maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
tunalojukumu la kutoa elimu juu ya Tanzania tuitakayo 2050 ili kuwaandaa vyema
wananchi wote kutoa maoni yao ambayo yatachangia kwa asilimia 100 katika
kuiandaa Dira 2050,”amesema Mafuru.
Amesema tume inatoa wito kwa wananchi wote kushiriki katika
kutoa maoni yake kwa kutoa majibu kuhusu dira hiyo.
Amesisitiza kuwa maoni ya kila mtanzania yanathamani kubwa
katika kuandaa dira hiyo hivyo ni vyema kwa kila mtu kushiriki ili kupata Dira
itakayokidhi matarajio na mahitaji ya Taifa.
Aidha Mafuru amevitaka vyombo vya habari nchini kuripoti
hatua zote za dira kwa kuandaa vipindi vya elimu na kuandaa mahojiano
yatakayoendeshwa na tume ili kuongeza uelewa na ushiriki wa umma.
“Vyombo vya habari vinapaswa kuruhusu na kuunda njia kwa
wananchi kueleza maoni yao katika vyombo vyenu waweze kuuliza maswali na kutoa
maoni juu ya Dira 2050 tunaahidi tume tutafanya kazi kwa karibu na waandishi wa
habari pamoja wadau wa maendeleo na mwananchi mmoja mmoja,”amesema.

Post a Comment