********
Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki, Dk Shogo Mlozi amefariki dunia.
Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson amesema hayo leo
Alhamisi Juni 13, 2024 kabla ya kuanza kwa kikao cha 47 cha mkutano wa Bunge la
bajeti huku akisema taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
Dkt. Tulia amesema ““Leo asubuhi tumepokea taarifa
kwamba Mh. Dkt. Shogo Richard Mloz ambaye tulimchagua kuwa Mbunge wa Bunge la
Afrika Mashariki hatunae tena, hii ni taarifa ya awali tutakapopata taarifa za
ziada tutawataarifu tusimame kaa dakika moja tumpe heshima zake za mwisho”

Post a Comment