********
Mtu mmoja ameuawa, 200 wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 100 wamekamatwa kote nchini Kenya, wakati polisi walipozima maandamano ya kitaifa dhidi ya mipango ya serikali ya kuongeza kodi.
Rex Kanyike Masai alifariki jijini Nairobi kutokana na kile kinachoaminika kuwa jeraha la risasi usiku wa Jumatano (Juni 20) huku Polisi wakisema ingelifanya uchunguzi wa kifo hicho.
Muungano wa mashirika ya kutetea haki za binaudamu umesema serikali ya Rais William Ruto inalenga kukusanya dola bilioni 2.7 kupitia kodi za ziada.
Waandamanaji wanaitaka serikali kuachana kabisa na mswada huo, wakisema utaudidimiza uchumi na kuzidisha ugumu wa maisha kwa Wakenya.
Lakini Shirika la Fedha Duniani (IMF) linasema serikali ya Kenya inahitaji kuongeza mapato yake ili kupunguza nakisi ya bajeti na viwango vya ukopaji.
ccDWkiswahili
Post a Comment