Mwenyekiti
wa Chama cha Kijamii (CCK) Taifa David Daud Mwaijojele akizungumza na mwandishi
wa habari hizi ofisini kwake Magomeni jijini Dar es salaam..
...................
NA MUSSA KHALID
Mwenyekiti wa Chama cha Kijamii (CCK) Taifa David
Daud Mwaijojele amewahamasisha Watanzania kutumia fursa ya kujitokeza kwa wingi
kushiriki kujiandikisha kwenye Daftari Ia Kudumu Ia Wapiga
Kura muda utakapo fika ili waweze kwenda kumchagua kiongozi aliyebora
wakati wa uchaguzi.
Mwaijojele amesema hayo jijini Dar es salaam wakati
akizungumza na kituo hiki akieleza msimamo wa chama chao katika kuhamasisha
wanachama kushiriki katika zoezi hilo ambalo hivi karibu Tume Huru
ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kusogezwa mbele kwa zoezi Ia uboreshaji
wa Daftari Ia Kudumu Ia Wapiga Kura hadi tarehe 20 Julai, 2024 badala ya tarehe
01 Julai, 2024 iliyopangwa hapo awali.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa kujitokeza
kwao kwa wingi itawasaidia kurekebisha taarifa zao kwa usahihi kwani malengo
yote yanayowekwa ni kwaajili ya kulijenga taifa la Tanzania.
Awali akizungumzia kuhusu mipango ya
chama cha CCK ni kuhakikisha watanzania kwanza wanaishi kwa uzalendo ikiwemo
kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.
‘Sisi CCK tunahitaji mifumo mizuri ya
kuwaletea wananchi maendeleo na vyakula hivyo lengo letu pia ni kuhakikisha
mtanzania anafurahia maisha na uchumi anafanya kilimo chenye tija cha kuwalete
maendeleo’amesema Mwaijolele
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa
kuwepo na utulivu nchini ndio utasababisha kuleta maendeleo hivyo amewataka
wanasiasa kukubaliana na matokeo zitakapofika nyakati za uchaguzi.
Amesema CCK ndio chama pekee
kitakachowawezesha wananchi kuwa na maendeleo katika maeneo hivyo amewataka
muda utakapofika wahakikishe wanachagua watu sahihi kwa muda sahihi kutoka
chama cha kijamii.
Akizungumzia wanasiasa ambao wameahidi
maendeleo na hawakutekeleza katika mitaa,Kata au Majimbo yao,ni vyema wananchi
wakafanya maamuzi sahihi kwa kufanya mabadiliko katika nafasi hizo.
Katika Hatua nyingine Mwaijolele
ameipongeza serikali kwa kufanya mambo mazuri kwa ajili ya kuibadilisha nchi
hii huku akisema kuwa licha ya hayo yote haitajiki kiongozi mzembe katia
utendaji wake wa kazi.
Amewataka watanzania zinapofika nyakati za uchaguzi wabadilike kwa kuepuka kupokea zawadi kutoka kwa wanasiasa badala yake wahakikishe wanachagua watu sahihi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Post a Comment