Mkadiriaji
Majenzi kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Elias Kissamo wakati akizungumza
kwenye mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu namna
ya kusuluhisha migogoro inayohusu sekta
hiyo ambayo yameratibiwa na Baraza hilo ambayo yanafanyikia jijini Dar es
salaam.
Jaji Mstaafu wa Mahakama kuu ya Tanzania Dkt Fauz Twaib akitoa mafunzo maalum kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu namna ya kusuluhisha migogoro inayohusu sekta hiyo ambayo yameratibiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo yanafanyikia jijini Dar es salaam.
Mkadiriaji Majenzi kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Anitha Mallewo akifuatilia kwa makini mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu namna ya kusuluhisha migogoro inayohusu sekta hiyo ambayo yameratibiwa na Baraza hilo ambayo yanafanyikia jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya wadau ambao wameshiriki kwenye mafunzo maalum ya kujengewa uwezo kuhusu
namna ya kusuluhisha migogoro inayohusu
sekta Ujenzi ambayo yameratibiwa na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ambayo
yanafanyikia jijini Dar es salaam.
Imeelezwa
kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluh Hassan imekuwa na
mchango mkubwa katika kuhakikisha usuluhishi wa migogoro katika sekta ya ujenzi
unafanyika kwa kufata taratibu zinazoheshimika ndani na nje ya nchi.
Hayo
yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mkadiriaji Majenzi kutoka Baraza la
Taifa la Ujenzi (NCC) Elias Kissamo wakati akizungumza kwenye mafunzo maalum ya
kuwajengea uwezo wadau wa sekta ya ujenzi kuhusu namna ya kusuluhisha migogoro inayohusu sekta hiyo
ambayo yameratibiwa na Baraza hilo.
Kissamo
amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kuwa na elimu ya kufahamu
namna ya kufanya utatuzi wa migogoro katika sekta ya ujenzi nje ya mahakama.
Aidha
Kissamo amesema Baraza la Taifa la Ujenzi limeundwa kwa ajili kuangalia
maendeleo ya ujenzi nchini ikiwemo kuwa na njia sahihi za kusimamia katika usuluhishi
migogoro.
‘Baraza
linasimamia usuluhisi na sio msuluhishi kwani linachagua wasuluhishi ambao wapo
kwenye mpangilio wanaosaidia katika kusuluhisha’amesema Kissamo
Awali
akizungumza Jaji Mstaafu wa Mahakama kuu ya Tanzania Dkt Fauz Twaib amesema
kutokana na kuwepo kwa migogoro imeonekana kuwe na haja ya kuwa na mfumo
mbadala mbali na wakimahakama kwa ajili ya kutatua migogoro.
‘Kuna
mambo mengi ambayo unaweza kuyaepuka kwa kutumia mfumo mbadala mmoja wapo ni
kujaribu kupunguza muda ambao utatumika kutatua migogoro kwani unapokwenda
mahakani utachukua muda mrefu zaidi kwani kuna mfumo wa kukata rufaa ambayo
inapoteza muda lakini pili mahaka ina utaratibu lazima uufate ili uweze kutatu
migogoro’amesema Dkt Twaib
Dkt
Twaib amesema kuwa wale ambao wanafanya kazi za Abitration mara nyingi wana
ujuzi na uzoefu katika hiyo fani ikiwemo katika matumizi ya nyenzo katika
ujenzi na gharama zake.
Kwa
upande wake Mshiriki wa mafunzo hayo rehema Mtulya ambaye ni Wakili wa serikali
kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa serikali amesema mafunzo hayo yatamsaidia katika
uendeshaji wa mashauri ya usuluhishi katika kazi zake za kila siku.
Pia ametumia fursa hiyo kutoa ushauri kwa wadau mbalimbali kuhudhuria mafunzo hayo kwani yataweza kuwasaidia katika kuepukana na migogoro kwani kwani katika mikataba mbalimbali inawagusa wananchi.
Post a Comment