***********
Na Mwandishi Wetu
Ngariba huyo anaishi Katika kijiji cha Masanga ,kata ya
Nyamwale, wilayani Tarime Mkoani Mara aliachana na shughuli hiyo tangu mwaka
2015 huku akikiri alifanya hivyo akiamini yupo sahihi.
Dkt. Henga alichukia uamuzi huo baada ya kutonywa na Asasi
ya Kupinga Ukeketaji (ATFGM) iliyoko mkoani huko alitaka kujua sababu ya Bhoke
kutekeleza hilo ilihali ni kinyume cha seheria.
Ameelezea kuhusu kutekeleza biashara hiyo, Bhoke alisema
jamii ya Wakurya wanaheshimu na kuenzi ukeketaji na endapo angeachana na
shughuli hiyo mapema angeweza kupoteza maisha.
Amesema alikuwa anafanya hivyo ili kuwasaidia mabinti waweze
kuolewa bila shida na kujipatia fedha
ambazo zimemsaidia kujenga nyumba mbili na kusomesha watoto.
"Gharama ya kulipia zoezi la ukeketaji ni Sh 10,000 na hiyo ni kwa miaka ya 2008 na kwa
wakati huu gharama inafika mpaka Sh 20,000 kwa msimu wa ukeketaji huwa
tunakeketa zaidi ya mabinti 200 na wazazi wao lazima walipie fedha na
zinagawanywa kwa wazaee wa Mila na Mangariba.
"Nilikuwa sijui kama kukeketa ni kosa kisheria jamii ya
huku wanaamini binti asipokeketwa anakuwa hajatimia ndio maana hii mila badoa
inaendelea huku kwa kifupi huu ni mradi wa mangariba kujipatia fedha"
alisema Bhoke akiwa nyumbani kwake
alipohojiwa na Dk Anna kuhusiana na harakati hizo.
Hata hivyo Dkt. Henga alionya kitendo cha baadhi ya
Mangariba kubadili ukeketaji kuwa mradi huku akiitaka jamii kutokuutumia kama
kivuli cha kujipatia fedha akisisitiza kitendo hicho ni ukatili wa kijinsia na
kinakatisha ndoto za mabinti wengi.
"Jambo hilo
limekuwa likisababisha madhara mengi ikiwemo kukatisha masomo, ndoa za
utotoni,vifo kwa watoto hasa wakati wa kujifungua pamoja na kuchochea magonjwa
mbalimbali" amesema Dkt. Henga
Picha mbalimbali za
(PICHA ZOTE NA JOHN SIMWANZA WA LHRC)




Post a Comment