***********
KUKOSEKANA kwa mitaji
,tatizo la sera ni changamoto ambayo inawakumba wabunifu kufikia malengo yao.
Hayo yamebainishwa leo
mapema jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Sahara adventures,Jummanne Mtambalike
wakati akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia Sahara Sparks mwaka huu
ambao inatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Semptemba mwaka huu.
Mtambalike amesema kwa
kipindi cha miaka 9 ya kuwepo sahara wamebaini wabunifu wanakosa mitaji ambayo
ingewasaidia katika kukamilisha kazi.
"Katika miaka
tisa yapo makampuni yamefanikiwa lakini tumeona wabunifu wanachangamoto masuala
mitaji pamoja na kutokuwa na sera,lakini sera linakwenda kufanyiwa kazi na
mamlaka husika"Amesema Mtambalike.
Aidha,Mtambalike
akizungumzia Sahara Sparks mwaka huu inatarajia kukutanisha wabunifu mbao
watakuwa na jukumu la kujadili mipango mbalimbali ambayo itaweza kuwasaidia
hapo mbeleni.
Kwa upande
wake,Samsoni mwena ambaye ni mkurugenzi wa menejimenti na maarifa kutoka Tume
ya Sayansi na teknolojia(COSTECK) amesema kwa kipindi cha miaka tisa
COSTECH wamekuwa wakishiriana na Sahara
kuandaa tukio hilo na kuwayataka makampuni kuja kushudia bunifu mbalimbali.
"Natoa wito kwa
wanaofadhili wajitokeze kuja kuona bunifu mbali"Amesema Mwena ambaye pia
alimwakilisha mkurugenzi wa COSTECK.
Post a Comment