TAKUKURU YATOA NENO KUELEKEA UCHAGUZI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU,) CP. Salum Rashid Hamduni akizungumza wakati akizindua warsha hiyo na kueleza kuwa mkakati utakaowekwa kupitia warsha hiyo utasaidia kupambana na rushwa kabla madhara hayajatokea. Leo jijini Dar es Salaam.

***********

Na Mwandishi wetu 

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imewataka Watanzania kujitenga na watu wanaotoa Rushwa ili kupata Nafasi za Uongozi.

Haya yanajiri Wakati Tanzania Ikijianda na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Ule Mkuu wa Uraisi, Wabunge na Madiwani mwaka 2025,

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam  na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Salum Hamduni wakati akifungua Semina ya siku tatu inayohusisha Wadau mbalimbali wa kukabiliana na Rushwa kutoka Asasi za Kiraia (AZAKI) na Asasi zisizo za Kiserikali (AZISE) kujadili namna ya Kudhibiti Vitendo vya Rushwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la (AZISE) Dkt Lilian Badi amesema wao kama Wadau muhimu wa wamejipanga vizuri kutoa elimu katika suala hilo muhimu hivyo ameiomba Serikali kuwaamini kufanya kazi hiyo kwa manufaa ya Taifa.

Nae Meneja wa Mipango wa (AZAKI) Michael Kyande amesema mikakati ya Taifa ya kukabiliana na Rushwa ambalo ni tatizo kubwa ni muhimu na kwamba wao wapotayari kujitolea na wanachohitaji kutoka kwa Serikali ni kuwaamini badala ya kuwachukulia kama maadui.

Warsha hiyo ya siku tatu pia inalenga kuwahusisha Viongozi wa Dini na Wahariri wa vyombo vya habari ambapo wanatarajia kuweka mikakati ya pamoja ya kuendelea kukabiliana na tatizo la Rushwa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU,) CP. Salum Rashid Hamduni akizungumza wakati akizindua warsha hiyo na kueleza kuwa mkakati utakaowekwa kupitia warsha hiyo utasaidia kupambana na rushwa kabla madhara hayajatokea. Leo jijini Dar es Salaam.

Bi. Neema Mwakalyelye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Salum Hamduni ili kufungua semina hiyo iliyofanyika leo Juni 26, 2024 kwenye Ofisi za Takukuru Upanga jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Bi. Lilian Liundi akizungumza kuhusiana na warsha hiyo na kueleza kuwa watatoa elimu kwa wanawake wagombea ili waweze kuripoti matukio ya rushwa pindi wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi. Leo jijini Dar es Salaam.


Wadau mbalimbali wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Warsha hiyo


0/Post a Comment/Comments