TAS YAMPIGIA MAGOTI SAMIA.

Mwenyekiti wa (TAS) Godfrey Mollel akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam akitoa tamko la kuchukuliwa kikatili na kupelekwa kusikojulikana mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novat (2)
Baadhi ya Watu wenye Ualbino Tanzania walioshikiri katika mkutano huo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

..................

Timothy Marko 

CHAMA cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) kimemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kukemea Vitendo vya Ukatili na kuwachukulia hatua za kisheria wanaojihusisha na biashara ya viungo vya watu wenye Ualibino.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam juu ya tukio lilotokea hivi karibuni la kinyama la kuvamiwa na kuchukuliwa kikatili na kupelekwa kusikojulikana Asimwe Novat (2) huko Muleba Mkoani Kagera Mwenyekiti wachama hicho Godson Molleli amesema kuwa Mama wa mtoto huyo alivyamiwa na genge la wahalifu mara baada ya wahalifu hao kudai Chumvi nyumbani mwa mtoto Asimwe Novat ambapo walimamia kwa minadi ya kuomba chumvi kutokana Ajali yanyoka wameipata wahalifu hao, mama wamtoto huyo na kumkaba koromeo mama wamtoto huyo,nakumchukua mtoto Asimwe novat nakutokomea kusikojulikana.

"Kitendo hiki nichakuchukiza, Chama cha watu Wenye Ualbino tunasimama na Asimwe Novat na Familia yake katika kipindi hiki  kigumu ambacho hatujui Mwenzetu yupo katika hali gani"Alisema Mwenyekiti wa (TAS) Godfrey Moleli.

Moleli aliongeza kuwa ni vyema serikali ikaongeza kasi ya Uchunguzi kwakutumia vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Chama hicho pamoja na wanakijiji wa mbale ilikuweza kuharakisha upatikanaji  wa mtoto huyo nakukamatwa kwa wahalifu hao.

Alisitiza kuwa Tukio hilo lilofanyika katika kijiji chambale linaikumbusha Serikali kuongeza jitiahada  za kukuza  uelewa kuhusu Albino na kufanya uchunguzi wa tukuo hilo kwa kina nakuwakamata watuhumiwa walio husika na tukio hilo nakuwa peleka Mahakamani. 

"Tunaiomba Pia Serikali kufanya  Uchunguzi ilikuwabaini waganga wanaofanya vitendo vya kupiga Ramli Chonganishi"Alisisitiza Moleli

0/Post a Comment/Comments