Na Mwandishi wetu dar es salaam.
WALIOKUWA wafanyakazi wa Mange Kimambi wamezindua kampuni yao mpya ya Reytox Pro Network itakayokuwa ikijiuhusisha na utoaji wa habari kwa njia ya mtandaoni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 10, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Reytox Pro Network Rehema Mussa maarufu kama Reytox amesema mtandao huo utakuwa na Website na kwamba kutakuwa na vipindi mbalimbali.
"Kwenye Website kutakuwa na stori mbalimbali, nitaandika uchambuzi na maoni yangu, nitakuwa naandika kwa maoni yangu na namna ninavyoona mimi. Kutakuwa na stori za siasa, burudani na nyingine nyingi," amesema Rehema.
Kwamba atakuwa na kipindi cha kufanya mahojiano kupitia kipindi chake cha Listen Up Podcast ambapo amesema kuwa wapaenzi na wafuatiliaji wake wawe tayari kukutana na mahojiano na wanasiasa mbalimbali.
Hata hivyo amebainisha kuwa hawatakuwa na upandeleo kwa Serikali katika utoaji wa habari zao bali watakuwa na habari za kila maeneo pasipo kujali tofauti zilizopo katika jamii, na kwamba watasaidia hata kutafuta haki kwa watu wanaoonewa na kunyanyaswa.
Ameongeza kuwa wao watakuwa wakisafisha wale waliochafuliwa na watu wengine kwa kuhakikisha wanatafuta ukweli wa taarifa husika ikiwemo zinatozuhumu watu, kwa kuwatafuta wahusika na kubalansi taarifa hizo na kuweka ukweli hadharani na kuondoa mkanganyiko.
Hivyo amesema lengo kuu la kuanzisha mtandao huo ni kuhakikisha wanabalansi stori kwa taarifa zote ambazo wahausika wanapaswa kujieleza na jamii kujua ukweli.
Akieleza sababu ya kuacha kufanya kazi na Mange Kimambi Meneja wa Reytox Pro Network Canon Hassan ambaye alikuwa ndiye Mchalishaji wa Vipindi vya Mange Kimambi App, amesema ni kwasababu Mange Kimambi amekuwa akimtukana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hassan amesimulia kuwa, waliwahi kumshauri Mange wajikite kwenye masuala ya habari za udaku/umbea na kuepuka kujiingiza kwenye masuala ya siasa kwani ndiyo eneo ambalo walikuwa tayari wameshalishika vizuri kwenye soko lao la habari.
Hata hivyo hakukubaliana nao na hivyo kuendelea na siasa na kuendelea kumshambulia Rais jambo ambalo hata wao lilikuwa likiwaweka katika mazingira magumu ya ufanyaji.
Akieleza jambo ambalo hawawezi kulisahau walipokuwa akifanya kazi na Mange, kwamba ni pale vodeo ya Msanii wa Hip Hap Prof. Jay ilipopandishwa katika mtandao wa Mange akiwa hospitali jambo ambalo lilifanywa wakamate na kupelekwa kituo cha polisi na kuhojiwa.

Post a Comment