UVCCM YAIANGUKIA SERIKALI KUFUNGIA MTANDAO X


 ********

Na Magrethy Katengu

UMOJA wa vijana UVCCM kimeomba kufungiwa Mtandao wa kijamii X ambao umekuwa ukisambaza Maudhui yanayoshawishi mapenzi ya jinsia moja yaani Ushoga na Usagaji .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jinu 11, 2024 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Kawaida amewaomba vijana wa chama hicho kukemea juu ya matumizi ya mtandao wa Twitter  maarufu kama X nchini Tanzania kutokana na kubadilika kwa maudhui ya mtandao huo

 Kawaida amebainisha  kuwa hivi karibuni wamepokea taarifa ya kushtua kutokana na mtandao huo kubadilisha maudhui yake na kuanza kuruhusu kutumika kwa picha na video  za ngono maarufu kama ponogroph zenye kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja huvyo  amewasisitiza  walezi na wasimamizi wa maadili ya malezi ya vijana na watoto sio jambo jema kuanza 

"Kwanza hata jina lenyewe tu linalotumika limekua na maudhui yanayoendana na masuala ya ponograph, watoto wengi wanatumia simu na wanaingia kwenye mitandao, hivyo sio vizuri kutimika nchini kwetu bora tuonekane washamba lakini tukiokoa kizazi kijacho kiwe salama chenye maadili "amesema Kawaida.

Aidha amesema wao hawana shida na mtandao huo ikiwa wataondoa maudhui  yake basi siendelee kutumika ila kama haiwezekeni basi vyema serikali ikaufungia kutokana na kuzalisha maadili yasiofaa.

0/Post a Comment/Comments