WAKAZI WA BOKO MANISPAA YA KINONDONI WAILILIA SERIKALI UCHIMBAJI HOVYO WA MCHANGA

..........,......
WAKAZI wa Boko, Magengeni Manispaa ya Kinondoni wamepaza sauti zao kwa serikali kuhusu uhalibifu mkubwa unaofanywa na wachimbaji wa Mchanga maarufu kama chepe Katika eneo la Mto Nyakasangwe 

Wakiongea na mwandishi wa Habari Leo Katika mto huo wamesema Malori Makubwa yamekuwa yakishuka mtoni kubeba mchanga usiku na mchana bila kizuizi chochote

Saidi Mtemi wa Boko amesema awali Manispaa ya Kinondoni iliweka vizuizi vya nguzo ili kudhibiti uhalibifu lakini wachimbaji mchanga walivingo'a na kuendelea Kupitisha Malori hayo

"Tunaambiwa mto Nyakasangwe hauruhusiwi kuchimba lakini angalia ngema kubwa zinazopelekea nyumba kuvamiwa na maji nyakati za mvua na kuleta Gharama kubwa kwa serikali au Taasisi za Mazingira" alisema

Mwanaidi Yusuph anasema mamlaka husika zijitokeze kuja kunusuru Wananchi badala ya kukaa ofisini na makaratasi, anasema kinachoshangaza ni kuona uharibifu mkubwa na Serikali haishtushwi na janga hilo "Athari ni kubwa sana, Wananchi walio karibu na mabonde hatulali wakati mvua inataka kunyesha, tunaomba mamlaka husika kuja kunusuru mto huu muhimu" alisema mkazi huyo

Chanzo Cha habari zaidi kinataja kuwa wapi Wanasiasa wametajwa kama chanzo Cha kuwatetea wahalifu hao kwa kisingizio Cha kushinda Uchaguzi, mwaka 2020 alitokea mwanasiasa ambaye aliwaaruhusu watu hao kuchimba mchanga bila kujali athari zilizipo

Naye Awadhi Jambo Afisa Mazingira Manispaa ya Kinondoni amezungumzia sakata hili na kutoa wito kwka serikali za mitaa kuendelea kulinda vyanzo vya maji na uharibifu kwenye Mito, amesema serikali inachukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukamata magari hayo, lakini ifike wakati Wananchi pamoja na Serikali za mitaa wanashiriki Katika ulinzi badala ya kuweka mbele maslahi binafsi

Post a Comment