*********
Na Magrethy Katengu----Dar es laam
MCHAMBUZI wa Masuala ya Kisiasa Kijamii na kiuchumi Dkt. Dennis Muchunguzi amewashauri wananchi kufahamu kuwa suala la sakata la sukari lililoibuliwa hivi karibuni bungeni na Mbunge Luhaga Mpina kuhusu kampuni zilizopewa zabuni za kuagiza bidhaa hiyo litatolewa majibu na Spika wa bunge Dkt Tulia Aksoni hivyo waache ushabiki katika mitandao ya kijamii.
Hivi karibuni Bungeni jijini Dodoma Mbunge wa Kisesa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Luhaga Mpina aliibuka na hoja kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Serikali walikiuka Sheria ya uagizaji wa Sukari kupitia kampuni mbalimbali zikiwemo zilizosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma za mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari Juni 16, 2024 jijini Dar es Salaam, Dkt. Muchunguzi amesema kwa kufanya hivyo maana yake Mpina amefanya kosa kwani alitakiwa kusubiri majibu ya Spika Dkt. Tulia Ackson na Bunge kwa ujumla.
"Mimi binafsi sijamuelewa, nafikiri Mpina alipaswa kusubiri kauli ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuzungumza mapema maana yake amem 'priemt' Spika, je inamaana hana Imani na Spika," amesema Dkt. Muchunguzi.
Dkt. Muchunguzi amesema kwa kuangalia lugha na namna mwili wake ulivyokuwa akizungumza Mpina inaonyesha kama ana mambo binafsi dhidi ya Bashe hivyo akaamua kuyaleta hadharani badala ya kumalizana faragha .
Sambamba na hayo kuhusu kampuni nyingine kama za simu kuagiza Sukari, amesema kuwa sio ajabu kwani kampuni inajisajili kufanya shughuli nyingi lakini hufanya shughuli.moja haina kikwazo ina uwezo kufanya shughuli nyingine tofauti ikiwemo kilimo, inaweza pia kuruhusiwa kuagiza ili kukabiliana na upungufu wowote unaojitokeza ndani ya nchi .
Amesema, kampuni hizo kupewa kibali cha kuagiza Sukari ilikuwa ni kwa nia njema.
"Hivyo nchi inapokuwa kwenye Dharura ya upungufu wa Sukari inabidi utafakari ni namna gani unaweza kukabiliana na hali hiyo bila kukiuka Sheria," ameongeza Dkt. Muchunguzi.
Hata hivyo Dkt. Muchunguzi amewataka Watanzania kuwa watulivu juu ya Sakata hilo huku wakisubiri kauli ya Spika Dkt. Tulia wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani suala hilo halina haja ya kuwafanya wananchi kuwa na makundi na kuondoa imani kwa Spika

Post a Comment