Timothy Marko.
WANAWAKE Nchini wametakiwa kutumia fursa mbalimbali ikiwemo kuzalisha Bidhaa zenye Ubora iliweze kuziuza nje nakuisadia kuleta Fedha za kigeni Utakao chochea Uchumi Nchini.
Akizungumza katika Katika Kongamano la Uwezeshaji WCW kiuchumi (Women Creating Wealth) Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa biashara za kimataifa Ushirikiano wa Kimataifa Masuala yakiuchumi Balozi John Ulanga amesema kuwa Kumekuwa na Mahitaji Makubwa ya bidhaa za Asali na Vitenge katika Nchi ya Malawi nivyema Wafanyabiashara Wanawake kuichangamkia Fursa ya kibiashara.
"Nivema Wanawake Nchini kuchangamkia Fursa za kibiashara hususa bidhaa za Asali na Vitenge Nchini Malawi" Alisema Balozi John Ulanga.
Balozi Ulanga aliongeza kuwa Wanawake Wamekuwa wakichangia Pato lataifa Nchini kwa kiasi kikubwa.
Alisisitiza Wanawake wanaomchango Mkubwa katika Kuzalisha Ajira Nchini Mijini na Vijijini.
"RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa kukuza Biashara Afrika Mashariki na kuhamasisha Usawa wakijinsia nakukuza Elimu kwa wanawake "Alibaisha Balozi John Ulanga.
Naye,Mkufunzi wa Mafunzo ya Uwezeshaji Kibiashara WCW(Women Creating Wealthing) Sabrina Rashid amesema kuwa Wajasiliamal wanawake ni vyema wakaandika Mchanganuo wa Biashara ili kubaini Faida na Hasara .
Alisema kuwa Kama hutokuwa na kumbukumbu za kibiashara hutoweza kubaini ukuwaji wa biashara .
"Kama Wajasilimali ni Vyema Kujua Fedha yako imendawapi na imetumikaje ilikuweza kukua kibiashara"Alisema Sabrina Rashid

Post a Comment