WASANII NCHINI WAMETAKIWA KUFANYA KAZI ZENYE UBORA.

 

*********

 Na Timothy Marko

KATIKA kuhakisha wasanii nchini wananufaika kazi zao,ikiwemo kazi za Sanaa na Muziki,TAASISI ya Hati Miliki nchini (COSOTA) imekutana Leo na wadau kazi hizo ilikuweza kujadili vifungu vya kisheria vitakavyo mnufaisha Mwigizaji naMtunzi wa Kazi za sanaa.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Juu ya itifiki Bejing Treaty on Audiovisual Performance Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hati Miliki (COSOTA) Doreen Sinare amesema kuwa itafaki hiyo ita muwezesha Muigizaji na mmiliki wa Kazi za sanaa kuweza kunufaika na itifaki hiyo.

" Itafaki hii itamunufaisha Muigizaji kuweza kunufaika na KAZI ya Sanaa,COSOTA,na BRELA tutahakikisha haki bunifu Nchini zinalindwa"Alisema Afisa Mtendaji Mkuu COSOTA Doreen Sinare.

Mtendaji Mkuu COSOTA Sinare amesema mpango huo unalenga kulinda na kuwanufaisha wabunifu,wasanii,waigizaji na wasanii wa kazi za Sanaa.

Aidha Mtendaji huyo alisema kuwa mkataba huo unalenga kukuza kipato ,biashara na kuzalisha ajira zitokana na kazi za sana nchini.

Kwa upande wake mwakilishi waTaasisi inayoshughulika na Hakimiliki Barani Afrika(ARIPO) Muren Fondo ameeleza kuwa Taasisi hiyo yenye wanachama wakutoka nchi za Ghana,Africa Kusini,Zambia pamoja na Tanzania katika malengo yake kupitia mkataba wa umoja wa mataifa unaoshughulika na masuala ya utamaduni(UNESCO) takribani ajira milioni 20 za kazi za Sanaa Barani Afrika ni chanzo Cha mapato ya Taifa katika nchi hizo.

Naye Mwakilishi wa Idara ya Sanaa na Utamaduni kipitia Wizara ya Sanaa,Michezo  na Utamaduni Venance Mwamengo amesma kuwa wasanii wanatakiwa kuwa wabunifu kwenye kazi zao ili kuleta tija kwa Taifa ili kuchochea uchumi nchini.

Aliongeza kwa kusema jitihada za kukuza kazi za Sanaa nchini zimetokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutaka sekta ya Sanaa kuweza kuchangia Pato la Taifa,alieleza kuwa Hadi sasa asilimia 10 ya Pato la Taifa linatoka na kazi za Sanaa.

"Hatima yetu ili itimie ni lazima tushiriki kwa udi na uvumba ,Hatimiliki ndizo zitawafanya watu waweze kuheshimu  wasanii na kazi za Sanaa",alisema Mwamengo.

Mwamengo aliwashauri wasanii kushiriki katika kongamano la kikao KAZI Cha wadau wa ubunifu kujadili na kupokea Itifaki ya Beijing ili kuweza kutoa mawazo na maoni yatakayoboresha itifaki hiyo.

Alimalizia kwa kusema wasipozielewa itifaki hizo watashindwa kunufaika na kazi za Sanaa.

Katibu Mkuu wa waandishi wa Vitabu Tanzania Mwanawetu Mmuni amesema kupitia itifaki ya Beijing wasanii watanufaika na kazi zao na kusisitiza kuwa Serikali imefanya jambo jema kuleta Itifaki hiyo kwa wakati.

0/Post a Comment/Comments