WATU 7 WAKIMBIZWA HOSPITALINI MAANDAMANO KENYA

 

******

Vyombo vya habari nchini Kenya vimeripoti kwamba watu saba wamepelekwa hospitalini katika mji wa Homa Bay magharibi mwa nchi hiyo, kufuatia maandamano ya kitaifa ya kuipinga serikali.

Licha ya kuahidi kuuondoa muswada wa fedha unaozozaniwa nchini humo, waandamanaji nchini humo wameendelea kuandamana kuipinga serikali ya Rais William Ruto siku ya Alhamisi.

Hali iliripotiwa kuwa ya wasiwasi katika mji mkuu, Nairobi, ambako waandamanaji walitangaza kuelekea ikulu yaliko pia makaazi rasmi ya rais.

Kundi la kwanza la waandamanaji lilikusanyika mchana wa leo katikati mwa jiji la Nairobi ambako maduka mengi yalikuwa yamefungwa.

Picha za televisheni zilionyesha polisi wakitumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji huku kukiripotiwa milio ya risasi.

#Dwkiswahili

0/Post a Comment/Comments