.jpg)
********
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo
ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabinchi
Akizungumza jana tarehe 24 Juni, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma, Dkt. Jafo amesema
changamoto hiyo ya mazingira inamgusa kila mmoja hivyo ni muhimu wadau hao
kushiriki kikamilifu katika kukabiliana nayo.
Amewaomba
washirika wa maendeleo kupitia taasisi mbalimbali nchini na nje ya nchi kuweka
kipaumbele suala la hifadhi ya mazingira kwa kutenga kiasi cha fedha hususan
katika zoezi la upandaji wa miti.
Halikadhalika,
amewapongeza wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakishiriki katika kampeni
mbalimbali za mazingira Srikali
inahakikha kil mmoj anashiriki katika kukabiliana na athari hizo kwa
kuwaelimusha wannachi
“Wapo
watu ambao kiukweli wanaonesha nia ya dhati kabisa na mwamko wa kushiriki
katika kampeni za hifadhi mazingira lakini wanakosa rasilimali kwa ajili ya
kutekeleza shughuli hizo hivyo ni wajibu wetu kwa ushirikiano na taasisi
tuwasaidie ili waweze kuwafikia wananchi,” amesema Dkt. Jafo.
Aidha,
Waziri Jafo amesema kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa Tanzania
na dunia kwa ujumla, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya muda mrefu na muda
mfupi katika kukabiliana nazo.
Ametaja
mikakati hiyo ni pamoja na kuzinduliwa kwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka
2021 ambayo imeweka mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za
kimazingira katika maeneo mbalimbali nchini.
Vilevile,
Waziri Jafo amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuchagiza biashara ya kaboni
ili wananchi pamoja na wawekezaji kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi.
Amesema
Serikali iliandaa
Kanuni na Mwongozo wa Taifa wa Usimamizi wa Biashara ya Kaboni nchini kwa lengo
la kuweka utaratibu na masharti ambayo wadau na wajasiriamali wa biashara ya
kaboni watapaswa kuzingatia wakati wa utekelezaji wa miradi mipya na miradi.
Pamoja
na hayo, pia Dkt. Jafo amesema katika kuwezesha utoaji wa taarifa za hali za hewa
nchini ambazo zinagusa moja kwa moja eneo la mazingira, Serikali imewekeza
katika Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Amesema
kuwa taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawasaidia wananchi kujiandaa na hata
kujikinga au wasipate madhara makubwa wakati wa matukio ya kimazingira yakiwemo
vimbunga au mvua kubwa.
Post a Comment