WIZARA YA ARDHI KUONDOA VIKWAZO VYOTE VYA UPIMAJI


..............

WIZARA ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema itaondoa vikwazo vyote vya upimaji kwenye Maeneo yote yaliyopandana ramani isipokuwa yale maeneo yaliyotengwa kisheria ikiwa ni pamoja na hifadhi ya miundombinu kama mabomba ya Gesi, Maji na Umeme

Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar Es Salaam na Afisa Mipango Miji mkuu na Mratibu wa Ukwamuaji Upimaji Ardhi Paul John Mbembela Katika kikao kazi cha wanakamati kutoka Katika mitaa ili Kuweza kuwamilikisha Hati Wananchi kutoka Katika kata za Tabata, Liwiti, Kinyerezi, Bonyokwa, Kipawa

Amesema serikali ya awamu ya sita Kupitia Wizara ya Ardhi imeanzisha mradi wa Kukwamua upimaji uliokwama awali baada ya baadhi ya makampuni kushindwa kumaliza kazi ya upimaji wa vipande vya Ardhi kwenye makazi ya Wananchi 

Vikwazo vyote vinavyotokana na mwingiliano wa ramani wakati wa zoezi la upimaji vitaondolewa na Serikali bila Gharama

 

0/Post a Comment/Comments