AIRTEL YAKAMILISHA MTANDAO WA 4G KIGOMA NA GEITA ILI KUBORESHA USHIRIKISHWAJI WA KIDIJITALI

· Airtel yawasha mnara wa 4G Geita na Kigoma kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.


· Airtel yawaunganisha Wachimbaji madini na Wakulima chini ya mradi wa Digital Tanzania

· Airtel yakamilisha mtandao wa 4G Kigoma na Geita ili kuboresha Ushirikishwaji wa Kidijitali

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amefika mkoa wa Kigoma na Geita, ikiwa ni mpango wake wenye lengo la kukagua na kujionea utekelezaji wa ujenzi wa minara mipya ya mawasiliano inayojengwa na wadau wa mawasilaino katika mikoa mbalimbali chini ya usimamizi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF kwa kushirian na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali

Akiwa mkoani Kigoma kijiji cha Kumbanga leo Mhe, Waziri amekagua mnara mpya wenye teknolojia ya 4G uliojengwa na Airtel Tanzania na kuendelea na ziara yake ambapo wiki hii atakagua minara mingine miwili iliyojengwa na Airtel mkoani Geita- kijiji cha Nyakagomba na Busonzo. Katika ziara hiyo, Waziri aliipongeza Airtel Tanzania kwa jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kuinua na kusambaza mawasiliano ili kuziba mgawanyiko wa kidijitali katika jamii za vijijini ambazo hazijafikiwa na mawasiliano.

Minara hiyo mitatu ni sehemu ya mpango wa Airtel Tanzania unaofadhiliwa na UCSAF na Benki ya Dunia chini ya mradi wa DTP ambapo ujenzi wake unalenga kuwezesha na kuboresha mawasiliano katika maeneo ambayo hayajawawahi kufikiwa na huduma yeyote ya mawasiliano.

Airtel Tanzania, katika mpango huu wa kusambaza mawasiliano vijijini tayari imekamilisha ujenzi na kuwasha minara 84 ya 4G, ikijumuisha minara hii ya Kigoma -Kumbanga, Geita-Nyakagomba na Busonzo.

Akizungumza katika ziara hiyo maalum ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mheshimiwa Nape Nnauye, alisema kuwa serikali iliweka ruzuku ya ya shilingi milioni 100 na kwa kushirkiana na Airtel mnara huo utaleta faida nyingi.


“Huduma nyingi za serikali zinaenda mtandaoni na unaweza ukazipata ukiwa hapa hapa kijijini kwa kutumia huduma hizi za mawasiliano. Huu mnara ndio benk yenu. Mnaweza mkalipana, mkanunua, mkafanya mambo yote kupitia mnara huu,” alisema Waziri Nape.

Minara hii mitatu ya Airtel itabadilisha maisha ya wananchi wa maeneo haya kwani itawawezesha kupata huduma mbalimbali za kidijitali kupitia simu za mkononi ambazo sekta zao zimeunganishwa ili kutoa huduma kama vile elimu, afya na kilimo.

Kwa upande wake, mmoja wa wakazi wa Kijiji hicho, alieleza kuwa uwepo wa mnara huo umeleta unafuu kwenye mawasiloiano ya simu kinyume na ugumu uliokuwepo hapo awali.

“Yaani mawasiliano yalikuwa ya shida sana. Mpaka uweze kwenda uende kwenye kichuguu ndo upate kuwasiliana lakini kwasasa hivi baada ya kutuletea huu mnara sasa hivi tunawasiliana vizuri na maendeleo yanaenda vizuri,” alisema

Kwa upande wake, Meneja Mauzo wa Kanda ya Airtel Isack Kijuu alieleza kuwa uanzishaji wa minara hiyo mitatu unadhihirisha dhamira ya Airtel Tanzania katika kuinua na kuleta mabadiliko chnanya maeneo ya vijijini kupitia teknolojia ya hali ya juu.

“Lengo letu la pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari ni kuboresha maisha ya Watanzania kupitia mpango huu wa Tanzania ya Kidijitali, tunahakikisha kwamba ushirikishwaji wa jamii katika kupata huduma za kidijitali si dhana ya kufikika tena. Ni jambo muhimu na wanastahili kupata mawasiliano ya uhakika," Kijuu alieleza.

0/Post a Comment/Comments