COSOTA YAWAMIZA WABUNIFU KUSAJILI KAMPUNI.

*********

WABUNIFU nchini  wametakiwa kujisari kampuni ili waweze kunufaika kwa mirabaa kupitia kazi zao.

Wito huo umetolewa na Afisa Elimu na Uhusiano kutoka Chama cha Hatimiliki nchini(COSOTA),Anita John,wakati akizungumza na waandishi kwenye Banda la COSOTA lilopo kwenye maonesho ya 48 ya Sabasaba.

Anita amesema mwaka 2022 kulifanyika kwa mabadiliko ya sheria ambapo ilianzishwa kampuni za kukusanya mirabaa ambayo itasimamia na wabunifu na wasanii wenyewe.

"Mwaka 2023 tulitoa leseni kwa kampuni ambayo hao watakuwa wanahusisha kukusanya mirabaha kupitia mziki"Amesema Anita.

Anita amesema bado kwenye kada za sanaa za maonesho,Kazi za Filamu pamoja sanaa za Ufundi bado hawajaanzisha kampuni zao.

"COSOTA tunatoa wito kwao kuanzisha Kampuni zao ili waweze kunufaika na kazi zao"Amesema Anita.

Hata hivyo,Anita,amesema hatua ya kuanzishwa kampuni hizo ni kutokana na maono ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ya kutaka kila msanii na wabunifu kunufaika na kazi zao.

"Rais tangu aingie madarakani ndoto yake ni wasanii kunufaika na kazi zao,ndio maana alikubali kufanyika mabadiliko kwa sheria ya hati ya Miliki sheria namba 7 ya mwaka 1999 na kuruhusu kwa kampuni hizi ambazo zitasimamiwa na wasanii wenyewe waweze kunufaika


 

0/Post a Comment/Comments