CRDB NA WATER ORG KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA MAZINGIRA TANZANIA


*******

Benki ya CRDB imesaini mkataba wa makubaliano na shirika la Water.Org la Marekani unaolenga kuboresha upatikanaji wa maji safi na mazingira safi katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mkuu Uendeshaji, Bruce Mwile amesema kuwa makubaliano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Benki ya CRDB ambayo inaelekeza katika kutoa suluhisho bunifu ili kukuza ustawi kwa jamii.

Mwile ameeleza kuwa kupitia ubia wa kimkakati na Water.Org, Benki ya CRB inakwenda kufanya uwezeshaji katika maeneo mbalimbali ikiwamo utafiti na ufadhili wa miradi ya maji na usafi wa mazingira, mikopo ya miundombinu ya maji na usafi, na huduma ya bima 

ya maji kukinga na majanga yanayoweza kuharibu miundombinu.Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Water.Org Afrika, Eng. Francis Musinguzi Water.Org amesema kuwa ushirikiano huu unalenga kwenye kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguka. Pamoja na hayo aliongezea kuwa utawezesha kuanzishwa kwa miradi endelevu ya maji na usafi.

Makaubaliano ambayo Benki imeingia na Water.Org ni mwendelezo dhamira ya kuchangia ufikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs), hususan Lengo namba 6, ‘Maji Safi na Usafi wa Mazingira’.





0/Post a Comment/Comments