DADA WA KAZI ALIYEDAIWA KUMCHINJA MTOTO MBARONI


 ******

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanamshikilia Clemensia Mirembe, anayetuhumiwa kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali maeneo ya shingoni, mtoto Malick Hashim (6), anayeishi eneo la Goba Kinzudi, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Kamanda Muliro kwa umma aliyoitoa leo Jumatatu, Julai 22, 2024 inaeleza upelelezi wa tukio hilo ulianza mara moja na jana Jumapili saa 4:00 usiku walimkamata mtuhumiwa huyo aliyekuwa mfanyakazi wa nyumbani akiwa amejificha kwenye pagala, maeneo ya Goba Kizudi.

Mtuhumiwa anahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.


0/Post a Comment/Comments